Rais John Magufuli |
CHARLES MULLINDA
VITA inayopiganwa sasa baina ya vikosi vya wanamgambo mamluki wa wazungu dhidi ya wapiganaji shupavu na wenye uzoefu katika medani za vita vya kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepamba moto.
Ni vita ngumu. Inagharimu uhai wa wanajeshi na raia. Wapiganaji wa CCM wanaoongozwa na makomandoo wa kike na kiume waliofuzu kwa viwango vya juu kabisa mafunzo ya vita vya kisiasa vya hovyo na kistaraabu na kwa upande mwingine wana mgambo mamluki wa wazungu, wanatumia silaha za kisasa na za kale kushambulia na kujihami. Wanatunguana kweli kweli, tena bila huruma.
Silaha zinazotumiwa na wana mgambo mamluki wa wazungu ni matusi, kashfa, uzandiki, uongo, upotoshaji na kuwavizia wapiganaji wa CCM kuwanyofoa roho zao ili wanyamaze milele. Wanajeshi wa CCM wana silaha nyingi sana lakini wamekwishatumia aina mbili tu; moja ni kumwaga sera na kunadi ilani ya chama chao kwa wananchi na pili kuomba kura kwa upole na unyenyekevu.
Vita hii kali imeingia katika vitabu vya historia ya siasa za Tanzania kwa sababu tangu kuasisiwa kwa Taifa hili haijapata kupiganwa na kwa namna ya pekee imewavutia walimwengu kuifuatilia na hasa mabeberu wanaofadhili vinyamkera wao kwenye uwanja wa mapambano.
Leo ni siku ya 10 tangu risasi ya kwanza ilipofyatuliwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya CCM, Rais John Magufuli pale uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuashiria mwanzo wa vita.
Tangu kufyatuliwa kwa risasi hiyo, wanajeshi vijana na wenye misuli ya haja wamekuwa wakiwashambulia kwa nguvu wana mgambo mamluki wa mabeberu wa kizungu. Wanawauwa kama kereng’ende.
Tayari mwana mgambo mkuu wa jeshi la mamluki ameishajeruhiwa na makomandoo wa CCM. Wapiganaji vijana wa Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli wamemsababishia majeraha ya mwili na akili wapinzani wao.
Ameanza kusikika akitoa amri zenye matege katika uwanja wa vita. Juzi aliamuru vijana wa msalaba mwekundu walioko mstari wa mbele wakitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa vita wakusanye vifaa vyao ndani ya dakika 15 watoweke vinginevyo atawashambulia. Amechanganyikiwa.
Tathimini ya kuudhi ya kichokonozi ya vita hii inaonyesha kuwa wana mgambo mamluki wa wazungu wamepwaya kwenye uwanja wa vita. Makamanda wao wameanza kwenda nje ya nchi kutafuta misaada.
Kundi la wana mgambo linaloongozwa na mwana mgambo mkuu limechakazwa vibaya na kikosi cha makomandoo wa CCM kinachoongizwa na Amri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.
Yeye mwenyewe Rais Magufuli yupo mstari wa mbele, anaongoza vijana wake huku anashambulia. Alianzia Dodoma ambako hakupata upinzani hata kidogo kwa sababu hiyo ni ngome yake kisha aliingia Singida ambako alifyeka wanamgambo mashoga wa wazungu bila huruma. Sasa yupo Geita, kote alikopita ameacha maumivu kwa mamluki.
Wana mgambo wa wazungu wapiga propaganda ambao kundi lao lina wanahabari mahili na wasomi nalo limezidiwa mno. Kikosi namba mbili cha makomandoo wa CCM kinachoongozwa na Komandoo wa kike kutoka Zanzibar, ndicho kikosi hatari zaidi dhidi ya wana mgambo mamluki wa wazungu.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan |
Kikosi namba mbili cha makomandoo wa CCM kinachoongozwa na Komandoo Samia kimechakaza vinyamkera wa wazungu Mkoa wa Morogoro na baadaye Pwani na kilipoanza kuelekea upande wa kusini kumkabili jasusi muuaji mwenye roho mbaya, jasusi huyo katoroka, kakimbilia kwa waarabu kuomba msaada.
Kundi la wana mgambo wa ardhini ambalo liko mstari mbele katika siasa za majukwaani, wapiganaji wake wengi wameangamizwa na wengine wameachwa na vilema vya kudumu.
Wapiganaji mamluki kutoka nje ya nchi waliokodiwa kuja kuongeza nguvu, wengi wao wamekamatwa mateka.
Waliosalimika wamebaki na vilema vya maisha. Handaki kubwa la Mtwara sasa sio mahali salama pa kujificha kwa sababu limewekwa katika rada za CCM.
Mahali salama ni Mtaa wa Ufipa ambako kuna chuo cha kijeshi na mahandaki mengi yaliyochimbwa na wana mgambo kwa ajili ya kujificha nyakati kama hizi wanapopata vipigo vya nguvu.
Sasa mbiu ya mgambo imelia. Wana mgambo mamluki wa wazungu popote walipojificha baada ya kusambaratishwa na wapiganaji na makomandoo wa CCM, kimbieni nendeni handaki la Ufipa.
Isikieni mbiu inayowapa taarifa za Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya CCM kwamba hivi sasa yupo kijijini Chato amepumzika huku akipata hewa ‘fresh’ ya Ziwa Victoria kabla yajanyanyuka kuendeleza kipigo.
Ndiyo muda muafaka, jitokezeni nendeni Mtaa wa Ufipa mkajipange upya na kuganga majeraha yenu huku mkizirutubisha upya afya zenu kwa kutibiwa kwenye hospitali zile zile zilizojengwa na Rais Pombe.
Wana mgambo mamluki wa wazungu mkiwa mafichoni mtaa wa ufipa ambako mtaishi kwa takriban miaka mitano mkifunzwa taratibu na tamaduni za wapiganaji magaidi kabla ya kurejea uwanja wa mapambano kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, wasanii wa wapiganaji wenu watunge nyimbo mpya za kuhamasisha uzalendo na kuinua hamasa ya kila Mtanzania kuyatafuta mabadiliko ya maisha yake yeye mwenyewe badala ya kusubiri kutafutiwa. Labda itasaidia kutibu majeraha makubwa mliyoyapata katika mbongo zenu
Nyimbo hizo mziimbe kila asubuhi katika kipindi cha miaka mitano mnapokimbia mchaka mchaka kwa ajili kupasha joto viungo vya miili yenu vilivyojeruhiwa kwa vipigo vya kikatili vya wapiganaji wa CCM.
Handakini Mtaa wa Ufipa maofisa wakufunzi wa vita, wajielekeze zaidi kuwafundisha masomo ya sayansi ya siasa badala ya sayansi ya wizi wa kura na wasisahau kutilia mkazo ufundishaji wa somo la athari za kususia shughuli za kitaifa, mikutano ya Bunge, kuandamana andamana na kuheshimu mamlaka zilizoko madarakani.
Katika mwendelezo wa mafunzo hayo mapesi na ya awali, wakati wa mijadala jadilini kwa mapana na marefu ni kwanini makamanda wenu wana vimelea vya ushoga na kwanini mwanamgambo mkubwa ni mlevi sana wa konyagi.Jiulize kama hiyo siyo sababu ya kupigwapigwa kama kitenesi na wanapiganaji wa CCM.
Kwa ari ya kuyapigania mabadiliko ya kweli ambayo yamehubiriwa na viongozi wenu wana mgambo wa muda mrefu, tumieni pia muda wenu mkiwa handakini kujadili uadilifu wa viongozi wenu hao. Wawekeni katika mizani ya uadilifu mmoja mmoja mkianza na kamanda mkuu Mzee wa Konyagi kisha afuate mpenzi wa ushoga.