Tuesday, June 24, 2025
spot_img

TANROADS NA KISA CHA NDOTO ZA KAKAKUONA KWA WATANZANIA

 

Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Patrick Mfugale

NA MWANDISHI WETU

MAISHA ya wananchi wa Tanzania kwa kiasi kikubwa sasa yamebadilika. Miundombinu ya barabara na madaraja ya kisasa ambayo hapo awali Watanzania waliyaona kwenye picha na sinema zilizoandaliwa katika nchi za Ulaya na Amerika, sasa ipo nchini na kwa kiwango kikubwa imekuwa msaada kwa safari zao wenyewe na pia kusafirisha mazao na bidhaa za biashara.

Mabadiliko hayo ya maisha ya wanachi wa Tanzania yameenda sambamba na mabadiliko ya mwenendo wa uchumi wa Taifa. Uchumi wa Tanzania sasa unakuwa kwa kasi kubwa na tayari umekwishachumpa kutoka kwenye uchumi wa nchi masikini hadi uchumi wa kati, miaka mitano kabla ya matarajio.

Wataalamu wa uchumi wanaeleza kuwa kuchumpa kwa uchumi wa Tanzania kutoka ule wa nchi masikini hadi uchumi wa kati miaka mitano kabla ya matarajio kumewezeshwa pamoja na mambo mengine, ujenzi wa miondombinu imara na yenye kuvutia jambo linaloifanya nchi, kwanza kufikika sehemu zote lakini pia kuwa na mandhari ya kuvutia.

Haikuwa kazi rahisi kuyafikia mafanikio haya katika sekta ya ujenzi wa miundombinu. Wapo Watanzania waliotokwa jasho la damu na chumvi kuyawezesha na kinara wa utiririkaji jasho la kuigeza Tanzania kuwa mithili ya paradiso ni Rais John Pombe Magufuli ambaye kwa miaka mitano ya awamu ya kwanza ya utawala wake, ratiba yake ya kulala imebadilika, analala kwa saa chache na muda mwingi yupo kibaruani akichuruzikwa jasho.

 

 Rais John Pombe Magufuli

Wa pili katika hili, ni Wakala wa Barabara, (Tanroads) ambao mabadiliko ya kiutendaji katika taasisi za serikali yaliyoasisiwa na Rais Dk. Magufuli mara tu alipoingia marakani mwaka 2015  yaliwafanya wawe kama wanajimu kwa kutafasili ndoto za mnyama mdogo anayejulikana kwa jina la Kakakuona.

Kakakuona hutembea akiota kuwa akikutana na binadamu na kufanikiwa kukimbia kwa kasi ili binadamu asimkamate kisha akajificha asionekane basi atakuwa na uwezo wa kibinadamu wa kufanya maendeleo makubwa katika maisha yake.

Binadamu nao, (baadhi ya jamii) huota kwamba wakimuona mnyama mdogo Kakakuona, basi kuna baraka mbele yao kwa sababu mnyama huyo haonekana hovyo hovyo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Tanroads ambayo ndoto za Kakakuona kutaka kukimbia kwa kasi kisha ajifiche ili awe kama binadamu na maendeleo yake imezifanya ziwe za kweli na kwa Watanzania waliokuwa wakiota siku wakikutana na Kakakuona basi kuna baraka inayokuja mbele yao, Tanroads imezigeuza ndoto zao kuwa kweli.

Ukweli huu umo katika kazi za kutukuka zilizofanywa na Tanroads kwenye ujenzi wa madaraja ambayo sasa yamegeuka kuwa vivutio vya utalii kwa watanzania wenyewe na hata baadhi ya wageni kutoka mataifa ya nje kutokana na muonekane wake wa kuvutia. Mbali na hilo, ndoto za watanzania katika baadhi ya maeneo ambako kulikuwa na matatizo makubwa ya kufika na hata uhai wa watu kupotea kwa sababu ya kukosa madaraja, hali hiyo sasa haipo, madaraja yamejengwa na hapa chini ni orodha fupi ya madaraja hayo.

DARAJA LA MAGUFULI


Kwa mujibu wa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dorothy Ntenga, Daraja la Magufuli lililojengwa katika Mto Kilombero liligharimu zaidi ya shilingi bilioni 50 ambazo zote zilitolewa na Serikali.


Kwamba ujenzi wa daraja hilo umezingatia viwango vilivyowekwa kwenye mkataba na mkandarasi ambaye ni kampuni ya M/S China Railway 15 Group Corporation.

Daraja hilo linarahisisha shughuli za usafirishaji wa mazao, ufugaji na madini katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

Ilikuwa ndoto ya muda mrefu kwa wananchi hao kupata daraja na wakati likijengwa, mmoja wa wakazi wa maeneo hayo, Zainabu Mtalanga alipata kumwambia aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Profesa Makame Mbarawa kuwa;  “Tunaishukuru serikali kwa ujenzi wa daraja hili kwani limekuwa mkombozi kwetu wananchi wa Wilaya za Ulanga na Kilombero.


“Hapo nyuma vifo vingi vimetokea pasipo kutegemewa wakati tukitumia kivuko kufuata huduma za kijamii wilaya jirani ambapo kuna huduma zote za muhimu.”

DARAJA LA MAGARA


Taarifa ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Manyara, Mhandisi Bashiri Rwesingisa, kuhusu ujenzi wa Daraja la Magara inaeleza kuwa ujenzi wake uligharimu zaidi ya shilingi bilioni 12

Lilijengwa na Mkandarasi M/s China Railway Seventh Group likiwa na urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4 na linaunganisha Hifadhi ya Taifa ya Manyara na Tarangire kupitia Mayoka, pamoja na kuunganisha mashamba makubwa ya mpunga na miwa yaliyopo ng’ambo ya pili ya Mto na Masoko ya Babati na Arusha.

Daraja la Magara ni kichocheo cha ukuaji wa utalii na uchumi  katika Mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla likiwa umbali wa KM 21 kutoka Mbuyu wa Mjerumani katika barabara kuu ya Babati – Arusha na sasa linawezesha kuvuka Mto Magara katika barabara ya Mkoa ya Mbuyu wa Mjerumani – Mbulu yenye urefu wa KM 49.

DARAJA LA MOMBA



Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Ndelalutse Karoza analieleza daraja hilo kuwa ni kiunganishi cha mkoa huo na Mkoa wa Songwe kwa upande wa Bonde la Ziwa Rukwa na limejengwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa 100.

Kwa mujibu wa Karoza, gharama za ujenzi wa Daraja la Momba  ni shilingi bilioni 17.7 na limejengwa na Kampuni ya ukandarasi ya Genjio Engineering Group Cooperation ya China

Karoza anasema ujenzi wa daraja hilo ni muhimu sana kwa mikoa ya Rukwa na Songwe pamoja na Tanzania kwa ujumla na kubainisha kuwa ukamilifu wa daraja hilo utawainua wananchi kiuchumi na kijamii ikiwemo kupunguza gharama za usafirishaji wa mazao.

Daraja la Mto Sibiti lipo Iramba mkoani Sindiga. Lina urefu wa mita 83 na gharama za ujenzi wake ni shilingi bilioni 19.2

 DARAJA LA NYERERE (KIGAMBONI)


Lipo Kurasini jijini Dar es Salaam na linamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na NSSF.

Ni daraja la aina ya kuning’inia lililojengwa na Mkandarasi China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering Company. Lina urefi wa mita 680 na upana wa mita 27.5 na gharama yake ya ujenzi ni Dola za Marekani milioni 136

Daraja la Nyerere ndilo linalovuka mkondo wa kurasini jijini Dar es Salaam likiwa na njia sita za kupitisha magari. Daraja la Nyerere ndilo kubwa kuliko yote Afrika Mashariki na linavutia sana kutokana na kujengwa kwa ustadi. 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya