Monday, June 23, 2025
spot_img

MBOWE AWEZA KUFUNGWA HADI MIAKA MIWILI

 

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe anaweza kufungwa gerezani kifungo cha mpaka miaka miwili iwapo Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga ataondoa huruma yake dhidi ya kosa alilolifanya yeye na wenzake la kudharua kwa makusudi nembo ya Taifa.

Hilo limebainika katika uchunguzi wa Tanzania PANORAMA Blog kuhusu makosa yanayoangukia kwenye kifungu namba saba (7) cha sheria ya Nembo ya Taifa ambayo Mbowe na wenzake waliyafanya wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Chadema wa kumchagua mgombea urais na makamu wake Mwaka 2020, katika ukumbi wa Mlimani City, siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni zilizodumu kwa siku 60.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa katika mkutano huo uliohudhuliwa pia na Tundu Lissu ambaye kitaaluma ni Mwanasheria anayezijua vema sheria za nchi, Lazaro Nyalandu, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii ambaye pia anazifahamu vema sheria na Mbowe ambaye alikuwa Mbunge katika Bunge la 11 akishiriki kutunga sheria za nchi, aliliiongoza baraza hilo kuimba wimbo wa Taifa huku yeye na wenzake hao wakiongezea maneno ambayo hayapo kisheria kwenye wimbo wa taifa.

Kwa mujibu wa sheria, kitendo hicho cha Mbowe na wenzake ni uvunjifu wa sheria namba saba kwa kuufanyia dhihaka wimbo wa taifa hivyo alipaswa kukamatwa yeye na wenzake wote waliofanya dhihaka hiyo na kushtakiwa mahakamani.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga, mapema wiki hii ameeleza kuwa hakuamuru kukamatwa kwa Mbowe na wenzake kwa kutanguliwa na busara ya kutoleta sintofahamu katika taifa kipindi cha uchaguzi mkuu.

 

 


DPP, Biswalo Mganga

Kauli hiyo ya DPP Mganga imepata nguvu kubwa kutokana ukweli uliopo kuwa wakati wote wa kampeni na kipindi cha uchaguzi mkuu, maadui wa taifa na hasa mataifa ya mabeberu walilenga kuibua hekaheka ambazo zingezaa machafuko na kuifanya nchi isitawalike, yakiwatumia wanasiasa watanzania vibaraka wanaoishi katika mataifa hayo.

Katika hatua ya kushangaza, Mbowe ambaye haina shaka anajua kuwa alitenda kosa na anapaswa kushtakiwa lakini bado yupo huru, ameanzisha chokochoko zinazoashiria kumshinikiza DPP Mganga kutokuwa na huruma na wale wote waliotenda kosa la kudharau kwa makusudi nembo ya Taifa.

Chokochoko hiyo ya Mbowe imedhihirika mwishoni mwa mwezi uliopita baada kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chadema iliyoketi kiimla kusikiliza na kuhukumu wabunge 19 wa viti maalumu wa chama hicho, kwa kutamka maneno yenye mwelekeo wa kutaka mmoja wa wabunge hao aliyekuwa akishtakiwa kwa kosa kama hilo hilo alilolifanya Mbowe la kudharau nembo ya taifa, arejeshwe gerezani baada ya DPP kumuachia kwa mamlaka aliyonayo kisheria.

Julai 4, 2020, Mbunge huyo akiwa katika Kijiji cha Puma, Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida alitenda kosa la kuimba wimbo wa taifa huku akiongeza maneno ambayo hayamo kisheria kwenye wimbo huo huku akipandisha bendera ya Chadema.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya