Monday, June 23, 2025
spot_img

DC MURRO- ARUMERU SI SEHEMU SALAMA KWA WAHALIFU

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Wilaya ya Arumeru (DC) mkoani Arusha, Jerry Murro amesema eneo la kiutawala la wilaya yake si sehemu salamu kwa wahalifu kutekeleza vitendo vya kihalifu ya kujificha.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa kukabidhi fedha, zaidi ya shilingi milioni 70 kwa wananchi wa wilaya hiyo walizokuwa wamedhulumiwa na wengine kucheleweshewa stahiki zao na kampuni mbalimbali zilizowaondoa kazini, alisema kazi ya kulinda haki na kutetea maslahi ya wananchi ni moja ya majukumu ya msingi waliyopewa wakuu wa wilaya ya mteule Wao, Rais John Magufuli.

Fedha hizo zimepatikana baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza kutelekeza oparesheni ya kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watu na kampuni zilizowadhulumu wananchi.

DC Murro pia aliwaonya watu waliotenda uhalifu ambao baada ya kufikishwa TAKUKURU hukimbilia kwa viongozi wa juu wakiomba wawalinde kuwa mbinu hiyo haitawasaidia na pia aliwatahadharisha wanaume wakware waliotelekeza watoto bila kuwapatia matunzo kuwa wataanza kufikishwa TAKUKURU ili wang’atwe.

“Anayejua amekula pesa ya mtu, iwe kwenye ardhi, kwenye kutaperi magari, Arumeru sio salama kwake. Na sisi tutakwenda mbali Zaidi mpaka wa watu wanaotelekeza watoto tutawaleta TAKUKURU. Maana wanajua hawana sehemu ya kuwapeleka wanawaonea sana maafisa maendeleo ya jamii. TAKUKURU ng’ata, itawang’ata.

“Wapo watu wanaletwa TAKUKURU waaanza kuzunguka kwa viongozi. Mwenye dhamana na chombo hiki cha TAKUKURU ni Rais John Pombe Magufuli,” alisema DC Murro.

Mkuu huyo wa wilaya alisema watu wanaofikishwa TAKUKURU wakituhumiwa kutenda uhalifu kisha wanaanza kupigia viongozi simu wakiomba msaada wa kulindwa katika wilaya yake hawana nafasi.

“Ukiona mtu ameletwa TAKUKURU waachie TAKUKURU usiingilie. Sijakaa mtu kwenda kwa kiongozi lakini nenda kwa kiongozi ukiwa umebeba hela ya mtu uliyemuibia.

“Kama huwezi kwenda kwa Deo au Ruge beba hela ile nenda Dodoma kamtafute waziri ambaye ni rafiki yako au mkuu wa mkoa yeyote au mtu mwingine yeyote ambaye ni wa Chama Cha Mapinduzi uliye na urafiki naye mkabidhi yeye hizo hela azilete na sisi tutazirudisha kwa wananchi wanyonge,” alisema.

DC Murro alisema kuna tatizo linaloanza kuota mizizi la watu wanaokamatwa kuanza kukimbilia kwa viongozi kuomba kinga ya kutowajibika kwa makosa yao waliyoyatenda  jambo ambalo linapaswa kukomeshwa.

Aliipongeza TAKUKURU kwa kuendelea kukomboa na kurejesha pesa kwa watu waliotapeliwa na kudhulumiwa kwa njia ya ulaghai na wahalifu.

Nao wananchi waliorudishiwa fedha hizo wamemshukuru DC Muro na serikali ya Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazofanywa za kurudisha haki za wanyonge. SI SEHEMU SALAMA KWA WAHALIFU

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya