Saturday, December 28, 2024
spot_img

WEZI WAJA NA MBINU MPYA

 

NA MWANDISHI WETU

MAGENGE ya uhalifu wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam yamebuni mbinu mpya ya kutekeleza vitendo vya kihalifu pasipo watu walio karibu na eneo la tukio kubaini chochote.

Mbinu hiyo ni kuwateka abiria wanaokuwa wamepanda kwenye daladala kisha wahalifu hao huanza kupiga kelele kwa namna ya kushangalia na muziki ndani ya daladala hiyo hufunguliwa kwa sauti ya juu sana.

Katikati ya kelele hizo za muziki na ushagiliaji ndipo wahalifu huanza kushambuliwa abiria waliowapakia kwa visu na bisibisi kabla ya kuwapora fedha na mali wanazokuwa nazo kisha kuwatupa njiani.

Moja ya matukio hayo ya kuogofya lililoshuhudiwa na Tanzania PANORAMA Blog, limetokea Jumamosi, Oktoba 10, 2020 eneo la Kunduchi njia panda ya kwenda Hoteli ya Bahari Beach, ambako daladala lililokuwa na genge wahalifu zaidi ya 20 lilisimama na mmoja wa wahalifu hao akatangaza kuwa linakwenda Makumbusho.

Katika kituo hicho, walipanda abiria watatu akiwemo Mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na baada ya kupanda na daladala kuondoka, dereva alifungua muziki kwa sauti ya juu na wahalifu wakaanza kushangilia kwa nguvu kwa staili ya ushangiliaji wa mashabiki wa soka.

“Baada ya kufungua muziki kwa sauti ya juu na wao kuanza kupiga kelele, walitoa mapanga na bisibisi wakaanza kutushambulia. Abiria wa kwanza mwanamke ambaye alikuwa ameng’ang’ania pochi yake alikatwa panga mkononi, mkononi ukaning’inia akaachia pochi akaanguka chini wakabembe hadi nyuma ya gari wakaanza kumsachi.

“Mimi nikajaribu kumwambia dreva asimamishe gari kumbe ni mwenzao maana alichomoa upanga mkali akanielekezea huku akinitaka nitulie. Wezi wale wakanivamia na sikuwa mbishi wakanipora na kunichakaza kwa ngumi za kutosha bila kujali kuwa sikutoa upinzani wowote kwao,” alisema mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog.

Alisema gari hilo lilikuwa linaendeshwa kwa mwendo mkali na kabla ya kufika njiapanda ya mbuyuni abiria mmoja ambaye alikuwa amekatwa mapanga mara mbili  mwilini na kuporwa kila kitu alitupwa nje na kuachwa hapo kisha gari likaondoka kwa kasi tena.

“Baada tu ya kukata kona ya mbuyuni gari likashika mwelekeo wa Mwenge lilipunguza mwendo na mimi nikasukumwa nikatupwa hapo lakini nilifanikiwa kukariri namba na rangi za hiyo daladala, kwahiyo kwenye gari wakabaki na mateka mmoja mwanamke waliyekuwa wamemkata mkono” alisema.

Alisema alichukua bodaboda hadi kituo kidogo cha Polisi Mtongoni na kutoa taarifa ya kushambuliwa na kuporwa fedha na mali na kwamba gari hilo likifukuzwa na pikipiki litakamatwa kwa sababu amekariri namba zake na kwamba kuna abiria ndani amekatwa mkono lakini polisi walisema hawana uwezo wa kulifuatilia isipokiwa afunguliwe faili na suala lake litaanza kushughulikiwa Jumatatu.

Alisema alipewa RB namba KMT/RB/2428/2020 pamoja na PF3 kwa ajili ya kwenda kutibiwa na kuelekezwa kufika Kituo cha Polisi Kawe Jumatatu ya Oktoba 12, 2020, asubuhi ambako ataonana na mpelelezi wa kesi na taratibu nyingine kuendelea.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya