Friday, December 27, 2024
spot_img

SABUNI ILIYOPIGWA MNADA NA TRA SIYO SALAMA

 



NA MWANDISHI WETU

SABUNI ya Unga ambayo muda wake wa matumizi umeisha lakini imeuzwa kwa njia ya mnada na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) siyo salama hivyo haifai kutumiwa.

Hayo yameelezwa jana na Afisa Mwandamizi wa Shirika la Viwango (TBS), jina lake tunalihifadhi katika mazungumzo yake na Tanzania PANORAMA Blog kuhusu madhara yanayoweza kuwapata watu watakaotumia bidhaa hiyo.

Akijibu hilo, amesema ni kosa kuuza au kusambaza bidhaa ambayo muda wake wa matumizi umeisha na siyo salama kuitumia ingawa matatizo ya kiafya yanayoweza kumpata mtumiaji ni suala la kitabibu na inategemea kemikali zilizotumika kuitengeneza.

“Matatizo ya kiafya ni suala la kitabibu na inategemea kemikali gani kwa sababu sabuni zinatofautiana ‘composition’ ya kemikali lakini itoshe tu kusema tu bidhaa yoyote iliyo’expire’ haifai na siyo salama kwa matumizi na anayeuza hatendi haki,” alisema afisa huyo.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema wanaoweza kulizungumzia ni TBS.

Mapema mwezi huu, TRA imeuza kwa njia ya mnada shehena ya sabuni ya unga ambayo muda wake wa matumizi umeisha.

Shehena hiyo ya sabuni iliingizwa nchini kutoka nje na kukaa bandarini bila kulipiwa ushuru kwa muda mrefu kabla TRA haijaamua kuiuza.

Habari za uhakika zilizokusanywa na Tanzania PANORAMA Blog zimeonyesha kuwa shehena hiyo ina mifuko 1,800 ya sabuni ya unga aina ya AKO na imeuzwa kwa njia ya mnada na maafisa wa TRA huku wakijua kuwa wanatenda kosa linaloweza kuwa na athari mbaya kwa watakaoitumia sabuni hiyo.

Thamani ya sabuni hiyo ni sh milioni 300 na kabla ya kunadiwa ilikuwa imehifadhiwa katika bandari kavu (ICD) ya Kampuni ya Azam

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha kuuzwa kwa shehena hiyo ingawa kabla ya kuthibitisha alikanusha na kutaka atumiwe ushahidi.

Katika majibu yake, Kayombo alisema “Sasa bwana ni hivi. Ni kweli huo mzigo unaousema ni kweli ulikuwepo TRA. Ni kweli kabisa. Na mnada wake wa kwanza ulikuwa Agosti 24, 2020 lakini aliyeshinda hakuja kulipa hivyo ikabidi ufanyike mnada mwingine ndiyo ukauzika

” Ni kama kulikuwa na pande mbili zilizokuwa zikiushindania kwa sababu yule mnunuzi wa kwanza hakuja kulipa hivyo ikabidi ufanyike mnada mwingine ndipo shehena ile ikachukuliwa kwa sh. milioni 21.5.”

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya