Friday, September 12, 2025
spot_img

MAJALIWA AKABIDHIWA CHETI YA UBUNGE RUANGWA

 

MBUNGE Mteule wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akipokea cheti cha ushindi wa ubunge wa Jimbo la Ruangwa kutoka kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo hilo, Frank Chonya (kushoto)  kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya  ya Ruangwa, Oktoba 29, 2020. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)


MWANDISHI WETU

MBUNGE Mteule wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa amepokea cheti cha kumtambulisha rasmi kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.

Alipokea cheti hicho Alhamisi, Oktoba 29, 2020 kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ruangwa, Frank Chonya katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

Akizungumza mara baada ya kupokea cheti hicho, Majaliwa amesema anamshukuru Mungu kwa kuwezesha yote na kuwafikisha hapo na kuwavusha salama kipindi cha kampeni kwa karibu miezi miwili

Majaliwa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa, alisema kipekee anashukuru vyama vya siasa wilayani humo kwa kumuamini na kuthamini maendeleo.

“Sisiti kusema vyama vya siasa vimeendelea kuthamini maendeleo ya wilaya yetu. Lakini katika hili, niseme kwamba tumeliweka mbele sana suala la maendeleo ya wilaya yetu. Ninawashukuru sana.”

Alisema kupatiwa cheti cha kumtambua rasmi kuwa mbunge mteule hadi atakapoapishwa, kumetokana na imani yao kubwa waliyoionesha kwake na kuamua apite bila kupingwa.

“Leo niko hapa mbele yenu, nimemaliza muda wangu wa 2015-2020, mmenivumilia, mmenipa ushirikiano na mmenisaidia kuifanya kazi yangu vizuri. Ninawashukuru viongozi wote na wananchi wa Ruangwa kwa mchango wenu uliowezesha Ruangwa ipige hatua ya maendeleo. Mimi, mke wangu na watoto tunawashukuru sana.”

Alisema katika miaka mitano iliyopita, yako mambo mengi waliyofanya na katika kipindi hiki yako mambo yaliyobakia kama kupeleka umeme na maji vijijini. “Ninawaahidi kushirikiana nanyi ili kufikia malengo yaliyowekwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM.”

Aliwapongeza madiwani wote walioshinda katika kata zote 22 na kuwaahidi kuwa yuko pamoja nao kuijenga Ruangwa.

Mapema, akizungumza kabla ya kumkabidhi cheti chake, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ruangwa, Frank Chonya alisema jimbo hilo lenye kata 22, lilikuwa na watu waliojiandikisha kupiga kura 106,043 na lilikuwa na vituo 311 vya kupigia kura.

Alisema vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo ni CCM, ACT Wazalendo, CUF na CHADEMA.

“Kabla ya uchaguzi, kata saba, wagombea wake kutoka Chama cha Mapinduzi walipita bila kupingwa. Jana baada ya uchaguzi, CCM imeshinda kata 12, ACT kata mbili na CUF kata moja.” Alisema.

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya