NA CHARLES MULLINDA
KAMPUNI ya vinywaji ya Mfanyabiashara Bilionea, Said Salim Bakhresa (SSB) imeanza kuandamwa na kashfa za unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanywa na wasaidizi wa karibu wa mfanyabiashara huyo.
Taarifa za uhakika zilizoifikia Tanzania PANAROMA Blog kutoka vyanzo mbalimbali vilivyo ndani ya kampuni hiyo na kuthibitishwa na maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi, zimeeleza kuwa tayari faili la uchunguzi kuhusu moja ya kashfa hizo limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Changómbe, kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa hizo za kikachero zimemtaja moja kwa moja, Idi Mzee ambaye ni dreva wa Bilionea Said Bakhresa kuwa ndiye aliyefunguliwa faili hilo la uchunguzi na kwamba simu zake za kiganjani pamoja na ya mlalamikaji zinashikiliwa na polisi kwa uchunguzi.
Inadaiwa kwamba mtuhumiwa alimshawishi kimapenzi kwa ukwasi mkubwa wa fedha mwanamke aliyekuwa akifanya kazi baa ya Valle Inn (jina tunalihifadhi) iliyopo Changómbe, Dar es Salaam kabla ya kumpa masharti magumu.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na mwanamke huyo zimedai kuwa Idi Mzee alimtaka mwanamke huyo awe anakutana naye akiwa na mwanamme aliyemuandaa kwa ajili ya kufanya naye tendo la ndoa huku yeye akitazama na wakimaliza ndipo Idi naye hufanya tendo hilo na mwanamke huyo huyo.
“Hii kesi ya watu Bakhersa na huyo dada (anamtaja jina) kweli ipo polisi. Yule mwanamke kamshtaki Idi kwa unyanyasaji wa kingono lakini pia kwa kumfanyisha mapenzi na mbwa. Tatizo polisi wa Changómbe hata sijui kama mtaifuatilia watawapa ushirikiano si unajua tena inahusu ofisi ya mtu mkubwa.
“Yule Idi ana tatizo fulani linalofahamika kwa wafanyakazi wenzake wote na muhusika wake ambaye ni mkubwa wa pale pale anafahamika kwa hiyo hawezi kufanya tendo la ndoa mpaka kwanza aone wengine wanafanya ndiyo na yeye anaweza kufanya.
“Sasa alimwambia yule mwanamke awe anatafuta wanaume anawapa pesa anakwenda nao kwake wanashiriki naye wakimaliza ndiyo Idi naye anashiriki na mwanamke huyo.
“Baadaye akaanza kumwambia leo njoo na mzee sana, mara njoo na kivulana cha shule na kwa vile ana pesa na yeye anasema pesa hiyo anapewa na mtu wake Bakhresa, hakuna mtu mwenye njaa anayeweza kukataa.
“Katembea na wanaume wengi sana huyo dada aliokwenda nao kwa Idi na kama ni ugonjwa sijui wangapi wameambukizwa Mungu apishilie mbali, na hao wanaume aliotembea nao wamekwenda polisi wamehojiwa na wamekubali kuwa ni kweli walikuwa wanafanya naye hayo matendo machafu mbele ya Idi na hadi mbwa kaishawahi kumuingilia huyo dada mbele ya Idi. Sasa wanapambana kuizima hao wakubwa na ndiyo tunasubiri kauli ya polisi,”kileleza chanzo cha Habari.
Alipoulizwa jana Mlinzi Mkuu wa SSB, Charles Zuakuu kuhusu kashfa hiyo alibabaika kujibu ambapo alianza kusema hasikii vizuri anachoulizwa kisha akakata na kuzima kabisa simu yake.
Alipopigiwa baadaye alitaka kwanza atajiwe jina la mtu aliyevujisha siri hiyo na jina la mlalamikaji huku akikiri kuwa ni kweli Idi Mzee ni dreva wa Said Bakhresa.
Alipoulizwa Meneja Rasilimali Watu aliyejitambulika kwa jina la Rose Mtesigwa kuhusu kashfa hiyo naye alianza kwa kubabaika alipoeleza kuwa hamfahamu kabisa Idi Mzee na hana kumbukumbu ya kusikia jina lake mahali popote wala kufanya kazi katika Kampuni ya Bakhresa.
Alipoelezwa kuwa lengo la Tanzania PANORAMA Blog kuhoji ni kutaka kuthibitisha iwapo ndiye anayechunguzwa na polisi kwa unyanyasaji wa kingono, Mtesigwa alibadilisha kauli kwa kueleza kuwa Idi anayemfahamu yeye ameajiriwa na Kampuni ya SSB wakati yeye anasimamia wafanyakazi wa Kampuni ya Chakula (BFB)
“Hiyo skendo naifahamu vizuri sana na hata chanzo chenu cha taarifa nakifahamu sana sana tu mimi hapa ni HR na wakili wa kampuni pia. Lakini Idi sinaye mimi hapa yeye yupo SSB . nendeni pale mapokezi nampa maelekezo dada hapo chini atawapa namba za HR wa SSB yeye ndiyo ataweza kumzungumzia,” alisema Mtesigwa.
Hata hivyo simu iliyotolewa na mtu wa mapokezi ilipopigwa ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwale, alipopigiwa simu yake ilipokelewa na msaizidi wake aliyeeleza kuwa bosi wake yupo kwenye kikao na ilipopigwa tena baadaye alipokea tena msaidizi wake na kueleza kuwa kamanda huyo alimtaka mwandishi kufika ofisi kwake kuzungumzia suala hilo badala ya kupiga simu.