NA CHARLES MULLINDA
JESHI la Polisi linasubiri uchunguzi wa kitaalamu wa simu za mkononi
za Idi Mzee na mpenzi wake wa kike (jina limehifadhiwa) anayemtuhumu kumnyanyasa kingoni pamoja na kumfanyisha tendo la ndoa na mbwa.
Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Jumanne Mkwama ameiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa uchunguzi huo
utakapokamilika ndipo hatua nyingine zitafuata.
Kamanda Mkwama amesema kinachochunguzwa na polisi ni nani kati ya
wawili hao aliyevunja mkataba wa kuvunja uhusiano wa kimapenzi ambao
ulisainiwa baada ya kutoelewana kwao.
Alisema mambo mengine yanayolalamikiwa na mwanamke huyo dhidi ya Idi, ikiwemo kumfanyisha tendo la ndoa na mbwa pamoja na kukiuka makubaliano ya kumlipa kila anapofanya tendo la ndoa na mwanaume huku yeye akiangalia kabla ya kushiriki naye tendo hilo yatashughulikiwa na mahakama.
“Tunasubiri uchunguzi wa kitaalamu katika simu zao. Simu zao tumezipeleka kwa wataalamu, tunataka kujua ni nani kati yao aliyevunja mkataba walioingia kwa maandishi wa kuachana. Hayo mengine watajuana wenyewe mahakamani,” aliema Kamanda Mkwama.
Idi Mzee ambaye ni dereva wa Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB)
amefunguliwa jalada la uchunguzi katika Kituo cha Polisi Chang’ombe
Jijini Dar es Salaam akidaiwa kumshawishi kwa pesa nyingi mwanamke
mmoja aliyekuwa akifanya kazi ya uhudumu katika Baa ya Valle In iliyopo Chang’ombe ili afanye tendo la ndoa na wanaume mbalimbali kabla ya kushiriki naye tendo hilo.
Taarifa hizi zimethibitishwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo
waliofikiwa kwa mahojiano na Tanzania PANORAMA akiwemo mwanasheria na
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bakhresa Food and Beverage (BFB)
Rose Mtesigwa.
Katika mahojiano hayo yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake Kariakoo,
Mtesigwa alianza kwa kueleza kuwa hamfahamu Idi Mzee na hana
kumbukumbu ya kusikia jina hilo mahali popote wala mtu huyo kufanya
kazi katika Kampuni ya Bakhresa.
Baadaye alisema Idi anayemfahamu yeye ameajiriwa katika Kampuni ya
Said Salim Bakhresa (SSB) lakini yeye anasimamia wafanyakazi wa Kampuni ya
Bakhresa Food and Beverage (BFB) na kuelekeza akaulizwe SSB.
“Hiyo Skendo naifahamu vizuri sana na hata chanzo chenu cha taarifa nakifahamu sana sana tu. Mimi hapa ni HR na wakili wa kampuni pia lakini Idi sinaye mimi hapa, yeye yupo SSB. Nendeni pale mapokezi nampa maelekezo dada hapo chini atawapa namba za HR wa SSB yeye ndiyo anaweza kumzungumzia,” alisema Mtesigwa.
Mfanyakazi wa mapokezi makao makuu ya makampuni ya Bakhresa aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Abdalla alitoa namba kama ilivyoelekezwa na Mtesigwa lakini namba hiyo imekuwa ikiita bila kupokelewa.
Awali, Mariam Abdalla naye aliieleza Tanzania PANORAMA kuwa analifahamu suala hilo lakini alishangaa ni nani aliyelifikisha kwa waandishi wa habari.
“Dah! naona sasa siri za kampuni zimeanza kutoka nje. Lakini nawashukuru ninyi ni waungwana sana kwa sababu mmekuja kuutafuta ukweli japo inaonekana mmefikishiwa kila kitu. Ninyi ni wanaume bhana lichukulieni hili jambo kama wanaume. Haya ni kweli yapo na sisi tumekuwa tukisema siku yakitoka nje tutaaibika sana.
“Sasa ujue Idi ni dreva wa mzee Bakhresa mwenyewe kabisa, kweli nawashukuru kwa kupoteza muda wenu kuja walau kupata maelezo ya upande wa pili lakini nataka niwaombe kitu, mimi Idi mtu wangu sana, niacheni nimtafute maana siyo rahisi kumpata kwa sababu simu zake ziko polisi, mpaka saa nane nitakuwa nimempata ili naye kama mlivyo sema aje aseme ilikuwaje kuwaje kwa sababu yapo madai ya kweli ambayo siyo siri yanafahamika lakini kuna mengine huyo mwanamke katia chumvi sana,” alisema Mariam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwele hakuwa
tayari kulizungumzia suala hilo baada ya kupigiwa simu mara kadhaa
iliyokuwa ikipokelewa na msaidizi wake ambaye alipopokea mara ya
mwisho alisema bosi wake amemtaka mwandishi afike ofisini kwake
kuzungumzia suala hilo badala ya kupiga simu.