NA MWANDISHI WETU
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshutumiwa kuhusika moja kwa moja na tukio la mauaji ya kinyama ya kijana Bryan Mollel.
Kwa mujibu wa taarifa ya kulaani mauaji hayo iliyotolewa na Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Amani na Maendeleo (TAMA), Mkoa wa Songwe, Jackson Eliabu inawataja waliohusika na mauaji ya kikatili ya kijana Mollel kuwa ni viongozi wa Chadema ambao walimpondaponda kwa mawe hadi alipokufa.
Taarifa ya Eliabu inawataja wagombea udiwani wa Chadema wa Mkoa wa Songwe kuongoza mauaji hayo kwa sababu ya kulazimisha wapewe fomu nyingine baada ya kuharibu waliyokuwa nayo.
Sehemu ya taarifa hiyo inasomeka hivi; ‘Tumepokea kwa masikitiko mauaji yaliyofanywa na kuongozwa na wagombea wa udiwani wa Chadema mkoani Songwe waliyoyafanya hivi karibuni kisa kulazimisha kupewa fomu nyingine baada ya kuharibu fomu ya awali.
‘Taarifa zinaeleza kijana Bryan Mollel aliuawa na wafuasi na viongozi wa Chadema baada ya juhudi zao za kuhonga hela ili waruhusiwe kuendelea kugombea kushindikana.’
Taarifa ya Eliabu inaeleza zaidi kuwa mbali ya kutekeleza mauaji hayo ya kinyama ya Mollel, pia walitaka kumuua kijana mwingine ambaye aliokolewa na polisi akiwa ameikwishambuliwa na sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
‘Mbali na kumpondaponda kwa mawe pia walitaka kumuua kijana mwingine kabla hajaokolewa na polisi na sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya akiwa na hali mbaya.’ inasomeka taarifa hiyo.
Taarifa hii ya Eliabu ni mwendelezo ya madai ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakikihusisha Chadema na baadhi ya makada wake na mauaji wakiwemo viongozi wa juu.
Freeman Mbowe alipata kunyooshewa kidole akihusishwa na kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Zakayo Wangwe kilichotokea eneo la Pandambili mkoani Dodoma na alinusurika kushambuliwa na wananchi wa Tarime alipokwenda kuhudhuria mazishi yake.
Aidha, Chadema kimekuwa kikihusishwa na matukio mbalimbali ya mauaji katika shughuli zake za kisiasa ikiwemo mikutano na maandamano