Thursday, December 26, 2024
spot_img

TRA YAFAFANUA MASHARTI MAGUMU MNADA WA PIKIPIKI

 

Richard Kayombo

NA CHARLES MULLINDA

MAMLAKA ya Mapato (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu mnada wa pikipiki zilizonadiwa mapema wiki hii baada ya kukaa bandarini muda mrefu bila kulipiwa ushuru.

Imesema masharti yaliyowekwa katika mnada huo ni ya kawaida kulingana na aina ya mnada ikizingatiwa kuwa pikipiki hizo hazijalipiwa ushuru.

Akizungumza leo na TANZANIA PANORAMA Blog, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema pikipiki hizo ziliingizwa nchini zikiwa hazijaunganishwa na kukaa bandarini muda mrefu bila kulipiwa ushuru hivyo TRA ilichukua uamuzi wa kuzipiga mnada.

“Hizo pikipiki ziliingizwa nchini zikiwa hazijaunganishwa na zipo mara mbili. Kasha la kwanza lina vipande vya pikipiki 25 na la pili lina vipande vya pikipiki 100. Mmiliki wake alishindwa kuzikomboa hivyo zilikaa bandarini muda mrefu zikidaiwa kodi.

” TRA ikatangaza mnada ambao umefungwa jumatano wiki hii na masharti ni kwamba kwa sababu ziliagizwa kutoka nje ya nchi hivyo hazijasajiliwa hapa nchini,  mnunuzi alipaswa ama kununua ule mzigo wa pikipiki zote 25 au ule wa 100 na siyo moja moja na akishanunua anapaswa kuzisajili.

“Katika hali ya kawaida, mtu binafsi hawezi kuja kununua pikipiki 25 au 100 kwa ajili ya matumizi binafsi, ni lazima awe mfanyabiashara ndiyo maana yakawekwa hayo masharti kwamba ni lazima awe na namba ya mlipa kodi na awe na VAT Kwa sababu baada ya kuzinunua atapaswa kwenda kuzilipia kodi,” alisema Kayombo.

Aidha Kayombo alisema mtu yeyote mwenye wasiwasi kuhusu mwenendo wa mnada huo au masharti yaliyotumika, milango ya ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi au kupokea malalamiko.

Awali ilidaiwa na baadhi ya waliotaka kuzinunua pikipiki hizo kuwa TRA imeweka masharti magumu ya kuzinunua ili kumuwezesha aliyeziagiza kuweka watu wake wa kuzinunua kwa bei ya mnadani baada ya kushindwa kuzilipia ushuru.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya