NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imekamilisha ukarabati na upanuzi wa miradi ya maji katika Wilaya ya Nansio mkoani Mwanza kwa gharama ya sh bilioni 58.
Hayo yameelezwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Nansio jana katika uwanja wa Getrude Mongela.
Majaliwa ambaye yuko katika ziara ya kisiasa nchi nzima ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Rais John Pombe Magufuli, amesema kati ya fedha hizo, sh bilioni 13 zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo sh bilioni 10.9 za uboreshaji wa huduma ya maji safi mjini Nansio utakaonufaisha wananchi 108,653.
Amesema sh bilioni 2.1 zimetumika kwa ajili ya kuboresha huduma ya usafi wa mazingira mjini Nansio.
Ameitaja miradi mingine ya maji iliyokamilishwa na Serikali ya Rais Magufuli kwa gharama ya sh bilioni 1.3 kuwa ni ukarabati wa mradi wa maji wa Irugwa, mradi wa maji ya bomba ya Nansore, mradi wa maji wa Muriti/ Ihebo, upanuzi wa mradi wa maji wa Chabilungo na upanuzi na ukarabati wa mradi wa maji Kazilankanda