Thursday, December 26, 2024
spot_img

SERIKALI YA CCM YAJIVUNIA KUFUTA UTITIRI WA KODI SEKTA YA UVUVI

 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Bukima, katika mkutano wa kampeni uliyofanyika viwanja vya Bukima, wilayani Musoma Vijijini, Septemba 20, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imefanikiwa kupunguza utitiri wa kodi kwenye sekta ya uvuvi katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo yameelezwa jana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Bukima, Wilaya ya Musoma, mkoani Mara.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majita ambako maelfu ya wananchi walifika kumsikiliza Majaliwa akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM,  Rais John Magufuli, alisema ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2015 -2020 ilielekeza upunguzaji wa kodi kwenye sekta ya uvuvi, agizo ambali limetekelezwa kikamilifu na serikali ya awamu ya tano.

Majaliwa ambaye aliutumia mkutano huo kuwaombea kura mgombea ubunge wa Jumbo la Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo na madiwani wa wilaya hiyo, alisema serikali imefanikiwa kupunguza kodi kwenye malighafi na zana za uvuvi, kuwatambua wavuvi na kuwaweka kwenye vikundi kazi, hatua iliyosaidia kuongeza idadi ya vikundi hivyo kutoka 37 hadi 113.

“Ni kwanini tuliamua kuwaweka kwenye vikundi, ni kwa sababu inakuwa rahisi kiwafikia, kuwaelimisha na kuwahudumia. Hii imefanikisha idadi ya samaki wanaovuliwa iongezeke kutoka 415,000 hadi zaidi ya 800,000.

“Kiwango cha uvuaji samaki kimeongezeka kutoka tani 300 hadi 448,467. Kikubwa ninachowaomba ni kwamba, tumieni vyombo vya kisasa kuvua samaki ili kutunza mazalio yao,” alisema Majaliwa.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya