Thursday, December 26, 2024
spot_img

RORYA YAMWAGIWA BILIONI 5.8 ZA ELIMU BILA MALIPO

 

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetoa shilingi bilioni 5.8 kwa shule 151 za Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya kugharamia mpango wa elimu bila malipo unaotekelezwa na serikali ya awamu ya tano tangu ilipoingia madarani mwaka 2015.

Fedha hizi zimenufaisha shule za sekondari 31 na za msingj 120.

Akizungumza na wananchi wa Shirati kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira Obwere, Kata ya Mkoma, Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara, Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa alisema sh. bilioni 3.3 zilitolewa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya shule za msingi 120.

Majaliwa alisema fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ukarabati, masuala ya utawala, michezo, mitihani na posho kwa maafisa elimu kata na walimu wakuu.

Alisema kwa shule za sekondar 31, serikali ilitoa sh bilioni 2.5 kwa ajili ya fidia ya ada, chakula kwa shule za bweni na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule.

Majaliwa alisema serikali kupitia mpango wa lipa kutokana na matokeo (EP4R)  pia ilitoa sh bilioni 1.2 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule ambayo ni pamoja na ukamilishaji wa miundombinu ya madarasa, vyoo na nyumba za walimu kwa shule za msingi.

Alizitaja baadhi ya shule za msingi zilizonufaika na mpango huo kuwa ni Mori, Nyanduga, Buchuri, Kondo, Saye, Masonga, Kyaro, Kitembe, Bubombi, Oliyo B, Dagopa, Nyabi, Ratia, Kotwo, Muchirobi, Manyara, Ochuna na Nuamaguku.

” Kwa upande wa shule za sekondari zimetumika sh milioni 777.8 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo maabara, madarasa, mabweni na vyoo kwa shule za Bukama, Mirage, Ngasaro, Nyamunga, Buturi, Goribe, Nyathorogo, Nyamtinga na Waningo.

Waziri Mkuu Majaliwa yupo Mkoa wa Mara akifanya kampeni za kumuombea kura mgombea urais wa CCM, Rais John Pombe Magufuli na aliitumia fursa ya mkutano huo kuwaombea kura mgombea ubunge wa Jumbo la Rorya, Jafari Chege, mgombea udiwani wa Kata ya Mkoma, Ayoi Mussa Sonde na madiwani wengine wa wilaya hiyo.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya