Thursday, December 26, 2024
spot_img

IPENI KURA CCM INA ILANI MAKINI YA UCHAGUZI – WASSIRA

 

Wassira

NA MWANDISHI WETU

STEPHEN Wassira, Waziri Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, amewaomba wananchi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 kwa sababu kina ilani makini ya uchaguzi.

Wassira ameyasema hayo Septemba 21, 2020 katika mkutano wa kampeni wa CCM ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya CCM na pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mara uliopo Kata ya Nyamatare, Wilaya ya Musoma.

“Tukisema mkapige kura, nendeni mkapige kura kwa wagombea na vyama vyenye ilani ya uchaguzi, siyo kukipigia kura chama ili mradi ni safari tu ya kwenda kupiga kura. CCM inazo sera zake na ndiyo maana tunawaomba muwapigie kura wagombea wa CCM.

“Hatuwezi kumpa mtu kura za urais kwa sababu tu tumekutana njiani. Rais ni mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na mkuu wa majeshi. Tunamuombea kura Rais Magufuli kwa sababu amejaribiwa na ameweza,” alisema Wassira.

Alisema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa mkoani Mara, mojawapo ni kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa katika kipindi cha miaka mitatu, ujenzi ambao ulisimama kwa zaidi ya miaka 40.

Wassira alisema uamuzi wa kujenga hospitali hiyo ulipitishwa kwa azimio la Chama Cha TANU la mwaka 1974 ambalo lilithibitishwa na mkutano Mkuu wa TANU  mwaka huo huo.

“Hapakuwa na bajeti ya ujenzi, lilikuwa ni suala la kujitegemea kwa hiyo tulianza na michango ya soda ndiyo maana ujenzi wake umechukua muda mrefu kukamilika,” alisema Wassira.

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya