Fatuma Karume |
NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya uwakili ya IMMMA imemtupia virago mwanahisa wake, Fatuma Karume, maarufu zaidi kwa jina la Shangazi.
Barua ya kufukuzwa kwa Fatuma Karume, maarufu kwa jina la shangazi, ya Septemba 16, 2020 ambayo TANZANIA PANORAMA Blog imeiona imesainiwa na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai ikiwa na maelekezo yanayomtaka shangazi kufungasha virago vyake ndani ya mwezi mmoja.
Shangazi aliisambaza barua hiyo kwenye mitandao ya kijamii akiambatanisha na ujumbe kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho.
Katika andishi lake hilo shangazi anaandika kuwa amefukuzwa kwenye ofisi aliyosaidia kuijenga na kosa lake ni uanaharakati.
Shnagazi ambaye pia ni mwanaharakati amefukuzwa na washirika wake wa muda mrefu katika fani ya sheria baada ya kujihusisha na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
Aidha, Shangazi amepata kushambuliwa hadharani na mmoja wa wazazi wake kutokana na mwenendo wake wa kuwashambulia kwa lugha isiyokuwa na staha viongozi wakuu wa kitaifa na bila kujali kuwa baba yake mzazi amepata kuwa kiongozi mkuu wa Zanzibar.
Fatuma Karume |
Katika barua yake ya kumfukuza Shangazi Fatuma, Magai anaandika kuwa anaondolewa kwenye umiliki wa kampuni na akusanye vilivyo vyake katika ofisi hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Magai anaandika zaidi akielekeza kuwa Shangazi anapaswa kurudisha kila kitu alichonacho ambacho ni mali ya Kampuni ya IMMMA na pia kesi alizokuwa anazisimamia azikabidhi na hasa kesi ya Kampuni ya Shivacom na Vodacom.
Andiko la Magai linaeleza pia kuwa Shangazi atalipwa stahiki zake kwa mujibu wa sheria