Thursday, December 26, 2024
spot_img

BILIONI 3 ZAKARABATI SHULE ZA MSINGI

 

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imetumia shilingi bilioni 3.29 kukarabati na kugharamia shughuli za utawala, michezo, mitihani na posho kwa maafisa elimu kata na walimu wakuu kuanzia mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2019/2020.

Fedha hizo zimetolewa na serikali kupitia mpango wa elimu bila malipo unaotekelezwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli ambao hadi sasa umezinufaisha pia shule za sekondari 23.

Hayo yameelezwa jana na Kassim Majaliwa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika majukwaa ya kisiasa wilayani Ukerewe ambako amefika akiwa katika mfululizo wa ziara zake nchi nzima za kumnadi mgombea urais wa CCM, Rais John Magufuli.

Majaliwa amesema katika utekelezaji wa mfumo wa uboreshaji wa miundombinu ya shule wa lipa kutokana matokeo (EP4R) ulioanza kutekelezwa 2015 hadi 2020, sh milioni 309 zilitolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo na ofisi kwa shule mbalimbali zikiwemo Kalandero, Murutunguru na Kakerege.

Amesema kiasi kingine cha sh milioni 873 zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo na maabara kwa shule za sekondari mbalimbali nchini zikiwemo Bukongo, Pius Msekwa, Bwisya, Muruti na Lugongo.

Ziara hiyo ya Majaliwa ilimfikisha katika Kisiwa cha Bwisya kilichoko Kisiwa cha Ukara ambako alitembelea Kituo cha Afya cha Bwisya na kukagua wodi ya wanaume na ya wazazi.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya