Thursday, December 26, 2024
spot_img


 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaji Rajab Kundya (mwenye suti nyeusi) akifanya mahoajino na waandishi wa Uhuru FM – Amsha Amsha 2020, Suti katika Shamba la Maua la Mwekezaji raia wa Uholanzi.


NA PIUS NTIGA, MOSHI

TANZANIA imesifiwa kuwa ina sera nzuri ya uwekezaji ambayo imekuwa kichocheo cha upatikanaji wa ajira na ukuaji wa uchumi.

Hayo yameelezwa leo na mwekezaji Fons Nijenhuis katika mahojiano na Amzha Amsha 2020 ya Uhuru FM shambani kwake Dakau, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Ameema zaidi ya ekari 250 zinatumika katika uwekezaji wa sh bilioni 6  tangu mwaka 2003 na kufanikiwa kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 1,000 katika shamba la maua la Vasso.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka  2015/2020 iliyoahidi kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji kama njia moja wapo ya kuongeza ajira kwa Watanzania

Fons Nijenhuis, amesema uwekezaji huo umetoa ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo na pia umesaidia kuchangamsha eneo hilo kibiashara na hivyo kuinua Uchumi.


Aidha, amesema amefanikiwa kuwajengea uwezo wananchi wanozunguka shamba hilo ambao miongoni mwao wameanzisha kilimo cha maua wanayoyauza kwake.

“Ngoja nikwambie hapa mimi nimefanikiwa kufundisha ujuzi wananchi wapo kama 40 hivi hawa wote wana mashamba hapo nje na maua yao huwa wananiuzia mimi na huwalipa kiasi cha shilingi milioni kama moja hivi kila wiki wanaponiuzia” anasema Mwekezaji.

Kwa mujibu wa mwekezaji huyo kila wiki husafirisha zaidi ya tani 250 za miche ya maua nje ya nchi na sehemu ya fedha zake hutumika pia kufanya ukarabati wa huduma katika vijiji vitatu vinavyozunguka shamba hilo.

Amesema katika shamba hilo anatumia tani 500 za udongo ambazo huziagiza kutoka nchini Uholanzi na kwamba udongo wa hapa nchini hautoshelezi.

Aidha, amesema anaendelea kufanya mazungumzo na serikali ili kuangalia uwezekano wa kuwa anatumia udongo wa hapa nchini ambao unapatikana Wilaya ya Pangani, Mkoa waTanga ili pesa anayotumia kuagiza nje udongo ibaki hapa hapa nchini.

“Sehemu kubwa ya wateja wangu wapo nchini China na Uholanzi ambako huuza hii Miche ya Maua,” alisema

Kwa upande wake, Afisa Kilimo Halmashauri ya Moshi Vijijini, Mercy Urio amesema uwekezaji huo umeleta manufaa makubwa kwa jamii na Halmashauri ya Moshi vijijini na wananchi kwa ujumla wanajivunia uwepo wa mwekezaji huyo.

Nao wanufaika wa uwekezaji huo, Agnes Shofa, Justina Mushi pamoja na Benard Erasto wamesema kwa sasa maisha yao yamebadilika ukilinganisha na awali walivyokuwa kwani wamefanikiwa kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba mpya.

Naye meneja wa shamba hilo, Alany Njau, amevitaja vijiji vitatu vinavyonufaika na uwekezaji huo kuwa ni pamoja na kijiji cha Umbwe, Ucharo pamoja na Dakau na wamekuwa wakifundisha ujuzi kwa wananchi wa namna ya kupandikiza pia Vikonyo.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Alhaj Rajab Kundya, aliambatana na Amsha Amsha 2020 ya Uhuru Fm, katika shamba hilo amesema mafanikio yote yamepatikana kutoka na uongozi thabiti wa Rais Dk. John Magufuli na kusisitiza kuwa chanda chema huvikwa Pete.

Aidha, mkuu huyo wa Wilaya ya Moshi, amesema shamba hilo la maua ni moja ya mashamba 11 yaliyopo katika wilaya hiyo na  yameendelezwa vizuri kupitia vyama vya ushirika.

“Kuna changamoto kadhaa ambazo hujitokeza kwa mwekezaji huyo lakini tumekuwa tukikaa pamoja kuzitafutia ufumbuzi wa kina”Amesema DC wa Moshi.

Amesema wanafarijika kuona maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji na kilimo cha kutumia mvua kinapitwa na wakati na serikali inahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinatunzwa vizuri ili kuleta chachu katika kilimo cha Umwagiliaji.

Chama Cha Mapinduzi katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020 /2025 imeahidi kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika kilimo cha Kisasa cha biashara hususani ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya