Thursday, December 26, 2024
spot_img

WARAKA WA VIJANA WA ACT WAZALENDO KWA ZITTO, MEMBE MGOMBEA URAIS WA ACT NI ZITTO AU MEMBE

MWANDISHI MAALUMU
SISI vijana wa ACT- Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali tunaendelea kusikitishwa na mwenendo wa uendeshaji wa chama chetu ambapo mpaka sasa hatuelewi kampeni inaendeshwa vipi zaidi ya kuona kila kitu kiko kwa mtu mmoja.
Pale Mlimani City tena kwa mbwembwe, chama chetu kilimteua Ndugu Bernard Membe kuwa mgombea urais na akaahidi kampeni ya kishindo. Kiongozi wa chama naye akaahidi hivyo hivyo.
Cha ajabu na ambacho sasa tunahitaji majibu kwa chama ni badala ya mgombea huyo rasmi wa urais kufanya kampeni, sasa hivi tunamuona kiongozi wa chama Zitto Kabwe akifanya mikutano mingi ya kampeni kuliko hata mgombea urais.
Juzi tu Zitto Kabwe alikuwa Dar, akaenda Kigoma na tukamuona kwenye ndege za ATC akarudi Dar, akaenda Mafia, akaenda Mtwara sasa kaenda Kigoma. Swali huyu ndiye mgombea urais wetu mpya? Ameteuliwa kimya kimya? Mzee wetu Membe kapatwa na nini?
Hivi kwa ‘stratejia’ hizi zilizoshindwa mapema tukipata kura kiduchu tutaanza vurugu za kudai tumeibiwa kura? Na nani kama mgombea wiki nne sasa hayuko majukwaani badala yake anafanya mtu ambaye siyo mgombea na ‘kujibrand’ yeye.
Tena bahati mbaya ndugu Zitto wala hamwombei kura mgombea, yeye ni kuhangaika na Magufuli na CCM na kumsifu na kujipendekeza kwa Lissu wa Chadema. Hakika hivi ni vituko!
Zaidi sasa kiongozi wetu wa vijana naye akitoka Kigoma kama Zitto, Abdul Nondo anamzidi Membe eti naye kusafiri kwenda kuzindua mikutano ya wabunge nchi nzima.
Hiki chama hakina uongozi, hakina ‘stratejia’ na kimechoka katika umri mdogo sana. Tunasikitika. Yani tunaumia sasa sisi vijana tunaohangaika huku mitaani kukitangaza chama huku kiongozi wa chama na mgombea urais wakituahidi kampeni ya kishindo, ndiyo hii ya Zitto kuzunguka kula ‘per diem’ na Nondo aliyetoka chuoni mwaka jana kuwa ndiyo mwanasiasa wa kwenda kuzindua kampeni za majimbo na wakongwe wa siasa ndani ya chama kuachwa?
Tunahitaji majibu. Yaani ACT kimekuwa chama cha kikabila, utasikia Maalim Seif yuko Pemba, Zitto yuko Kigoma, mikoa mingine chama ziiiii. Inatuuma sana.
HUU NI WARAKA WA WAZI WA VIJANA WA ACT WAZALENDO. TANZANIA PANORAMA BLOG IMEUBEBA KUTOKANA NA UJUMBE WAKE MZITO KWA WANACHAMA, WAPENZI NA MASHABIKI WA ACT- WAZALENDO NA PIA KWA WATANZANIA WOTE.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya