RAIS WA TFF, KARIA |
DAR ES SALAAM
Kuna malalamiko kuwa ajira katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinatolewa kwa upendeleo na baadhi ya watu waliojiriwa hawana sifa huku wengine wakitajwa kuwa hawana vyeti ama wameghushi vyeti.
Taarifa kutoka ndani ya shirikisho hilo zimedai kuwa baadhi ya watu waliojiriwa bila kuwa sifa stahiki wana uswahiba wa viongozi wa juu wa shirikisho hilo.
Majina ya wanaodaiwa ajira zao hazikufuata taratibu
ni Loveness Issack ambaye ni Mhasibu, Chiku Badru – Mtunza Stoo, Maua Lubibi – Office Manager, Latifa Chijumba – Receptionist, Raymond Gweba – Desk Officer.
Wengine kwenye orodha hiyo ni Rose Msamila – Afisa wa Dawati la Wanawake, dereva binafsi wa Katibu wa TFF, Wilfred Kidao, ambaye ametajwa kwa jina moja la Yohana, Jackline Kamwamu – Katibu Muhutasi, Jonathan Kassano – Refa na kocha wa soka la ufukweni, Aron Nyanda – Afisa Masoko, Clifford Ndimbo – Afisa Habari, Bonifasi Pawassa – Afisa wa Soka la Ufukweni na Baraka Kiziguto – Afisa wa Kitengo wa IT.
Taarifa kamili ya utata wa ajira hizi itawajia hapa hapa.