Wednesday, December 25, 2024
spot_img

MeTL HAIJATELEKEZA AGIZO LA SERIKALI



DAR ES SALAAM

Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) inayomiliki mashamba ya Mkonge yaliyoko Tanga, bado haijatekeleza agizo la Serikali la kuyaendeleza kwa takribani miezi minne sasa.
Disemba 8, mwaka jana, MeTL ilipewa siku 24 na Serikali kuyaendeleza mashamba hayo yenye ukubwa wa hekta 9,418 ambayo miongoni mwake hayajaendelezwa na badala yake yamegeuka kuwa pori.
Naibu Waziri Mabula akiongea na wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi Korongwe

Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga na kubaini kuwa MeTL iliendeleza baadhi tu mashamba hayo baada ya kupata ilani ya kutaka kunyang’anywa.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa sekta ya Katani zinaeleza kuwa agizo la Serikali lililotolewa na Naibu Waziri Mabula, halijatekelezwa tangu mwaka jana ingawa kampuni hiyo iliandika barua serikalini ikieleza namna itakavyotekeleza kwa awamu uendelezaji huo.
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stephen Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Majimarefu ambaye aliambatana na Naibu Waziri Mabula katika ziara yake hiyo ya mwaka jana, alieleza kuwa MeTL ilimilikishwa mashamba hayo mwaka 2000 lakini tangu wakati huo ilishindwa kuyaendeleza kikamilifu.
Baada ya agizo hilo la Serikali, Ngonyani aliishukuru Serikali kwa kuiona kero ya ardhi jimboni kwake.
Tayari Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuyarejesha kwa wananchi mashamba ambayo hayajaendelezwa na wawekezaji ambao baadhi wanadaiwa waliyatumia kuchukulia mikopo benki lakini waliitumia kwa shunguli nyingine.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya