Wednesday, December 25, 2024
spot_img

> MCHOKONOZI

RAIS POMBE ANA JESHI LA KALE

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Rais Magufuli RAIS John Pombe anaweza kushindwa. Anaweza kushindwa kupata mafanikio ya kuridhisha katika mapambano dhidi ya ufisadi kwa sababu jeshi lake lina wapiganaji wa kale wanaokimbia mchakamchaka huku wakiimba wimbo wasiouamini. Yeye mwenyewe ni mpambanaji mzuri, anajua kuchora ramani ya vita, anajua kuhamasisha majeshi yake kwa nyimbo za kimapinduzi kama ule wa hapa kazi tu na anajua kuwatungua adui. Mafanikio aliyoyapata katika vita dhidi ya ufisadi si ya kupuuzwa na haina shaka ataendelea kuyapata. Lakini ili aendelee kufanikiwa hana budi kuachana na baadhi ya wapigana… more »

KESHO TUTACHEKWA PAMOJA NA KIKWETE

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Kikwete KILA ninaipoitazama Tanzania ya kesho ninawaona watoto wa watoto wetu wakitucheka kwa kushindwa kuiishi misingi ya utawala bora, kutofuata sheria za nchi, wanasiasa kuendekeza ulafi wa madaraka walioujenga katika misingi ya chuki, fitna, majungu na kuisigina Katiba ya nchi. Watoto wa watoto wetu ninaowatazama katika safu hii kwa jicho la kichokonozi, ninawaona wakihangaika kuperuzi nyaraka mbalimbali zilizotumiwa na watawala wetu wa sasa kuliongoza taifa letu ili ziwe msaada kwao katika kuchukua uamuzi lakini hawaoni inayowafaa. Ni chache sana zinasomeka bila kuacha maswa… more »

HISTORIA IANDIKWE UPYA SASA (1)

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Mullinda + Ratifa NI jambo la bahati mbaya sana kwamba wapo baadhi ya watu ambao husoma maandishi ya kichokonozi bila kuyaelewa na wapo pia wengine ambao husoma na kuelewa lakini husahau baada ya dakika chache. Wiki mbili zilizopita, niliandika katika safu hii nikieleza kiunaga ubaga hatari ya binadamu kupigana vita na Simba, wengi walisoma andishi lile, lakini waliolizingatia ni wachache, na wapo pia waliosoma na kuelewa lakini baada ya dakika chache walisahau walichokisoma. Hili linadhihirishwa na shangilio la kitoto la baadhi ya watu ambao baada ya kusikia taarifa za Mchokonozi ku… more »

ROHO IMEKUFA MWILI UNAISHI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Mullinda NIMEFIKISHIWA ujumbe wa kienyeji kuwa watu wanaojeruhi wenzao kwa vitu vyenye ncha kali hawafurahishwi na maandishi yangu. Ujumbe huo niliofikishiwa unaeleza kuwa maandishi yangu yanawaudhi wenye roho na miili ya kinyama wanaoishi katikati ya miili yenye roho zilizokufa. Hawayapendi kwa sababu yanawaudhi, wanayasoma kwa kujilazimisha kwa sababu yanavutia kusomwa lakini yanaudhi yanaposomwa. Wamekasirika. Maandishi yangu yanawafikirisha hadi uwezo wao wa mwisho wa kufikiri. Kwa sababu mwisho wa uwezo wao wa kufikiri ni kujeruhi wenzao kwa vitu vyenye ncha kali, nadhani hat… more »

KIBANDA HANA SHUKRANI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
KibandaNIMEPATA fursa ya kukaa kitako na Absalom Kibanda na kuzungumza naye mambo mengi huku anakotibiwa baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya na genge la wahuni wanaojijua. Katika mazungumzo yetu nimegundua kuwa Kibanda hana shukrani hata kidogo. Nafasi hiyo nimeipata baada ya kumtembelea nchini Afrika Kusini aliko sasa. Tumezungumza mengi sana lakini katika mazungumzo yetu hakuna hata mara moja Kibanda alitoa shukrani kwa watu wanaoonekana kuwa wema mno kwake wakati huu anapouguza majeraha aliyonayo. Kibanda hawashukuru wale wanaoonyesha kumpenda ghafla hivi sasa baada ya k… more »

WAMEMNG’OA KIBANDA JICHO LA MWILINI WAMEMUACHIA LA ROHONI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Kibanda NIKO nchini Afrika ya Kusini kwa takriban wiki moja sasa. Nimekuja kumjulia hali kaka, bosi na Mwalimu wa wachokonozi, Absalom Kibanda ambaye alivamiwa, akashambuliwa na kujeruhiwa vibaya na wahuni fulani ambao wanajijua . Kibanda alinipokea Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, yeye na mkewe na saa chache kabla sijaondoka Tanzania nikiwa uwanja wa ndege Dar es Salaam, alinipigia simu na kunitaka ninunue magazeti ya Mtanzania, Tanzania Daima na Raia Mwema, nimempelekee. Nilifanya hivyo. Nikiwa angani kuja Johannesburg, picha tofauti tofauti zenye sura ya Kibanda zilikuwa zikin…more »

NINAKUAMKIA KAKA ABSALOM KIBANDA

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Kibanda ABSALOM Norman Kibanda, ninakuamkia kwa lugha adhimu ya kichokonozi, shikamoo kaka. Ninakuamkia kwa upendo uliopitiliza wa kichokonozi huko kitandani kwa wageni ulikolala ukiuguza majeraha uliyoyapata baada ya kuvamiwa, ukashambuliwa na kujeruhiwa vibaya na genge la wauaji. Wanajijua. Waliokuvamia walikuchokonoa sehemu mbalimbali za mwili wako, wakakutoboatoboa bila huruma maungo yako kakamavu, wakakupondaponda kifua na kichwa kisha wakakusagasaga udongoni kabla ya kukutupa hapo walipokutupa ukiwa mahututi, hivyo hata ningekukuta hapo usiku ule nisingekuamkia bali ningek… more »

NINAKUAMKIA JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
J.K Nyerere MWALIMU Julius Kambarage Nyerere, ninakuamkia shikamoo. Habari za miaka 12 iliyopita? Ninatambua umetu‘miss’ sana watanzania wako ambao hutujakuona kwa muda mrefu sasa baada ya kuondoka bila kutuaga. Hukutuaga wala hatukukuaga kwa sababu ulifia mbali, ugenini kwa wazungu. Hao ndiyo waliokuona ukikata roho, wakakufunika macho na kuunyoosha mwili wako vizuri. Sisi watu wako tulipokea kiwiliwili chako na kukifukia ardhini. Basi. Inauma sana kwa mtu tuliyekupenda kutuacha bila neno la mwisho. Kama wewe ulivyotu‘miss’ nasi ni hivyo hivyo. Tumeku‘miss’ mno. Na amini us… more »

NIMEMALIZA FUNGATE NINATAKILIFU KUITALIKA SERIKALI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
KWA kawaida fungate hudumu kwa muda wa siku saba. Hili ni fungate la kawaida baina ya wanandoa ambao ni mume na mke. Kwa wachokonozi fungate ni mapumziko rasmi ya muda usiojulikana yanayolazimishwa na wakubwa ambao hushinikiza pande mbili zinazopingana kwa hoja na kutofautiana kimtizamo kuwa kimya kwa sababu ya woga wa kuumbuliwa na wakati mwingine kuepusha shari. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Mchokonoz. Kabla ya fungate, Mchokonozi alikuwa daraja muhimu kati ya watawala na watawaliwa na zaidi alikuwa na kazi ya kuwachokonoa watawala kwa wakati muafaka na kwa staili nzuri inayofur… more »

KWA SABABU YA UCHAGUZI 2010 MUNGU ATUJALIE MATESO NA KILIO

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
YAPATA miezi nane sasa tangu nilipowaonya wapiga kura wa Tanzania waliokuwa wakifurahia kupewa ubwabwa na maharage, khanga, tisheti na kofia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ili wawachague waliokuwa wakiwahonga kuwa si muda mrefu watakuwa wakinung’unika, wakilia na hata kufa kwa makosa yao wenyewe ya kutumia kura zao vibaya kwa kuchagua bora viongozi badala ya viongozi bora. Katika makala ile niliandika kufafanua yale ambayo nilikuwa nikiyaandika katika mfululizo wa makala zangu za maswali elfu lela na moja kwa rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete. Ingawa niliandika kwa lugha ny… more »

CHONDE CHONDE MPENZI SPIKA MAKINDA

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Makinda SIKUPATA kufiriki hata siku moja kukujadili kwa heri au kwa shari kiongozi wangu mpenzi wa Bunge, Spika Anne Makinda kwa sababu ya kuhofia kukutia doa, wewe mwenyewe na kiti chako cha uspika. Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana sikuwa na mpango wa kuhudhuria mkutano wa pili wa bunge la kumi ingawa ninawajibika kufanya hivyo. Kwa wasiofahamu sababu ya mimi kuhudhuria vikao hivi bila kukosa, niwafahamishe kuwa mimi ni mbunge wa kulazimisha niliyejiteua mwenyewe kuwawakilishi wachokonozi wote wa Tanzania katika chombo chao hiki cha kutunga sheria. Hata hivyo, nililazimika kuf… more »

SPIKA MAKINDA KUWADI WA UFISADI?

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Makinda LEO ni sikukuu ya maboksi (boxing day) watu wanapeana zawadi kwenye maboksi wakati wakiendelea kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristo, sikukuu kubwa kwa wakristu duniani kote. Kwa sababu ya ukubwa wa sikukuu hii, ofisi nyingi hasa za serikali zimefungwa. Hakuna kazi, wafanyakazi wanapumzika. Miongoni mwao ni wafanyakazi wa Idara ya Mahakama kubwa ambako siku chache zilizopita niliwasilisha ‘chaji shiti’ namba moja ya mwaka ujao wa 2012 dhidi ya polisi. Leo nilipaswa kuwasilisha ‘chaji shiti’ namba mbili ya mwaka 2012 dhidi ya polisi lakini kwa sababu mahak… more »

AKILI YA RAIS KIKWETE CHANGANYA ZA MBAYUWAYU

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Kikwete RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete ndiye kiongozi mkuu wa kaya yetu. Tunayatambua mamlaka aliyonayo, hatuna shaka hata kidogo na uelewa wake wa mambo hivyo tunapaswa kumsikiliza na kufuata ushauri anaotupatia. Kwa kulitambua hilo, ni mawazo yangu kuwa ushauri uliopata kuutoa mara kadhaa akiwaasa watanzania kupima kwa usahihi mawazo au ushauri wanaopatiwa na kisha wauchanganye na akili za Mbayuwayu ili kupata uamuzi sahihi, haupaswi kupuuzwa kwa namna yoyote ile. Tunapoenenda katika ushauri huu wa Kikwete, tunapaswa kuanza kwa kuchambua kauli zake ambazo hupasishwa na akili… more »

MBATIA POPO WA KISIASA ALIYECHUJA

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Mbatia HUWEZI kuandika ukurasa mmoja wa historia ya harakati za vijana katika kutafuta na kujenga mageuzi ya Taifa hili bila kuandika jina James Francis Mbatia. Huu ndiyo ukweli ingawa kwa baadhi yetu hatupendi kuusuikia. Nimeanza kwa kuukiri ukweli huu kwa sababu wahenga wana msemo wao usemao “mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.” Hivyo pamoja na ukweli kwamba sasa anaonekana kupwaya katika nafasi nyeti aliyonayo ya kiongozi wa chama cha upinzani. Mbatia ni miongoni mwa Watanzania waliojitolea sehemu kubwa ya muda na nafasi zao kushiriki harakati za ujenzi wa mageuzi ya ki… more »

‘POSTMORTEM’ YA KICHOKONOZI YA AKILI MBILI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Afande Barlow AKILI mbili za binadamu wawili zimeuchanganya ulimwengu. Zimefanya uchunguzi wa maiti kwa kupeleleza sababu ya kufo na kutoa majibu tofauti. Akili hizi mbili, zote zinasadikika kuwa zina akili, zinaaminiwa na walimwengu ndiyo maana wakazipa kazi hiyo nyeti ya kufanya uchunguzi wa maiti kwa kupeleleza sababu za kufa kwake. Kwa maana nyingine, akili hizi mbili zinaaminiwa sanakwa sababu kufanya uchunguzi wa jambo kama hilo sio suala la mzaha. Dosari iliyojitokeza ni kutoa majibu mawili tofauti katika uchunguzi wa maiti moja. Na katika uchunguzi huo hapo awali, akil… more »

CCM MWALIMU MZURI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Mkutano wa kampeni za CCM Igunga MWEZI mmoja wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga uliomalizika Oktoba Mosi umetuacha na fundisho kubwa la jinsi wanasiasa wetu hususan wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walivyo wa hovyo na wanavyopenda ukubwa kuliko kulitumikia taifa. Katika kipindi hicho tumeshuhudia jinsi wanasiasa wa CCM walivyo na pesa za kuhonga na kufanya kila aina ya anasa. Na kikubwa jinsi wanavyotumia vibaya madaraka tuliyowapa. Tumeona kwa macho jinsi walivyo mabingwa wa kuhonga na hata walivyo wazinzi wa kupitiliza kiasi cha kufanya ngono na wake wa wanasiasa wenz…more »

RAIS KIKWETE, HISTORIA ITATUHUKUMU (1)

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Kikwete RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete, siku nyingi zijazo baada ya kufa kwetu historia itatuhukumu. Wakati huo utakapofika, natabiri miaka alfu lela na moja ijayo, wajukuu wa wajukuu wa wajukuu zetu, watapokuwa wakisoma maandishi ya kichokonozi ya safu zenye akili za aina ya Mchokonozi, nikizitaja kwa uchache pamoja na Mchokonozi; Tuendako, Wazo Jepesi, Maswali Magumu, Usn’zibe Mdomo, Fikra zangu na Mtegemea Nundu ambazo nina hakika zitadumu na kudumu katika mioyo ya vizazi vingi vijavyo, watakuwa wakitoa hukumu dhidi yetu kulingana na maandishi, maneno na matendo yetu ya… more »

EDWARD LOWASSA, ASIPOKUBALI KUFA, AKAZIKWA HATAFUFUKA

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Lowassa KUNDI dogo la waombolezaji wa kisisasa limetawanyika katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, huku kila mwanakikundi huko aliko akiwa anatoa kilio cha nguvu za kukataa kuwa hakuna msiba wa kisiasa wa Edward Lowassa. Wana kikundi wa kundi hili dogo wametawanyika sehemu mbalimbali za nchi lakini sauti za vilio vyao ni kali na zenye kuudhi kweli kweli masikioni mwa watu. Wana sauti kali kwa sababu wanakula wanashiba. Kazi yao ya uliaji misibani inawalipa vizuri, hivyo wana uhakika wa kula na kusaza. Jamaa hawa waombelezaji ni maarufu sana hapa nchini kwa sababu wanafahamika … more »

KIKWETE ANAOGOPA, TUMTIE MOYO

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Jakaya Kikwete RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete amekumbwa na woga mkuu kiasi kwamba sasa anajiogopa hata yeye mwenyewe. Anaogopa kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wake. Hali hii si nzuri, tunapaswa kumsaidia kuondoka nayo. Kwa pamoja tunapaswa kumtia moyo. Tukimuacha, ataendelea kuogopa kwa kipindi kirefu. Atakuwa anaogopa kukutana na mimi rafiki yake, kisa, kiherehere changu cha kumwandama kili ahudhurie mdahalo wa wagombea urais. Atakuwa anaogopa kukutana na watu wanaomtaka sana kwenye mdahalo, na hasa atakuwa anaogopa kukutana na watu wenye akili. Sitaki jambo hili litok… more »

SIKIA HAYA YA MSHANA WA MAELEZO

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
NILIKUWA Dodoma mwezi uliopita, nilikuwa huko kwa zaidi ya wiki moja. Nilikwenda kuhudhuria uzinduzi wa bunge la kumi na shughuli nyingine kadhaa za kitaifa ikiwemo kuidhinishwa na bunge kwa jina la Waziri Mkuu wa n’gwe ya pili ya serikali ya awamu ya nne baada ya kuteuliwa na rais. Sambamba na shughuli hizo, nilikwenda kuburudika na watukufu wachache wa nchi hii. Nilikwenda kujumuika nao kula mapochopocho na kunywa mvinyo wa bei mbaya tukiwa katika mavazi nadhifu – suti – za bei mbaya na mkuki shingoni ambayo ni nadra sana kuvaliwa uswahili. Kilikuwa kipindi kifupi cha kuishi ma… more »

RAIS KIKWETE, DADA JOYCE MCHOKOZI

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
RAFIKI yangu Rais Jakaya Kikwete, ninaleta mashtaka kwako. Ninamshtaki Dada Joyce Mapunjo, ananichokoza. Ananitisha kwa kutumia kaukubwa ulikompa katika ofisi yetu. Mashtaka haya nayaleta kwako kwa nia njema kabisa, nataka umkataze hiyo tabia ya uchokozi kwa sababu akiendelea nayo, ataniudhi. Nikiudhika na mimi nitamchokoza. Ikiwa hivyo, tutakuwa tunachokozana na matokeo ya kuchokozana hayatakuwa mazuri. Rafiki yangu Rais Kikwete, uchokozi wa Dada Joyce ni huu; ametuma vijana wake aliona pale ofisini ulipomuweka waje wanifanyie fujo kwa kutumia mwamvuli wa ukubwa uliompa. Wame… more »

TUTAKUMBUKWA KWA KIFUNGO CHA SIKU 90

Charles Mullinda at M I K I T O – 6 months ago
Historia ya uhuru wa vyombo vya habari Tanzania, Afrika na ulimwengu kote haiwezi kusomeka kwa usahihi pasipo kuitaja Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Gazeti la Mtanzania toleo la siku ya Jumatano na safu ya Mchokonozi. Kwa sababu hiyo, Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Gazeti la Mtanzania toleo la siku ya Jumatano na safu ya Mchokonozi vitakumbukwa duniani miaka mingi ijayo kwa sababu ya kufungwa kifungo cha siku 90 na serikali. Hivi ndivyo imekuwa ikitokea duniani. Historia inaonyesha kuwa watu waliopata kufungwa au kushtakiwa kwa sababu ya kutetea ukweli, au taasisi iliyofung… more »

Previous article
Next article

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya