Wednesday, December 25, 2024
spot_img

> HABARI

RAIS WA TFF KUMMALIZA WAMBURA LEO?

Charles Mullinda at M I K I T O – 7 hours ago
Karia DAR ES SALAAM Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia ameitisha mkutano na wahariri wa habari za michezo, leo.Mkutano huo unatarajiwa kufanyika katika Hotel ya Sea Scape, iliyopo Dar es Salaam saa 4.00 asubuhi. Inatarajiwa kuwa, Rais Karia atautumia mkutano huo kutoa ufafanuzi wa tuhuma ambazo Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amezielekeza kwa taasisi anayoiongoza. Aidha, haina shaka kuwa Rais Karia atautumia mkutano huo kuzungumzia kwa kina uamuzi wa kumfungia milele, Wambura kutojihusisha na shughuli za michezo.

TFF ni kisasi au ufisadi?

Charles Mullinda at M I K I T O – 3 days ago
DAR ES SALAAM Mjadala mpya umeibuka nchini baada ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuadhibiwa kutojihusisha na soka milele. Wambura anatuhumiwa kughushi nyaraka na kuchukua fedha kinyume cha taratibu. Lakini Wambura amepaza sauti akisema kwanza waliomuadhibu hawana mamlaka hayo lakini pia hatua hiyo imefikiwa kwa sababu ya kukemea maovu ndani ya TFF? Wambura amekaririwa kuwa alihoji matumizi mabaya ya fedha za TFF. Wambura Kwamba yeye (Wambura) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya TFF alihoji matumizi mabaya ya shirikisho hilo linalodaiwa kutumia kiasi cha sh… more »

Mjukuu apanga mauaji ya babu yake kwa milioni moja

Charles Mullinda at M I K I T O – 4 days ago
RUKWA Mzee mwenye umri wa miaka 72 aliyefahamika kwa jina la Paul Kisiwa, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ng’ongo ameawa kwa kupigwa rungu kichwani. Mzee huyo aliuawa Machi 3, mwaka huu majira ya jioni katika Kijiji cha Kifinga kilicho Kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando ambaye amesema watu sita akiwemo mjukuu wa mzee huyo wanashikiliwa na polisi. Kamanda Kyando alisema mjuu wa mzee Kisiwa alikubali kuchukua sh. Milioni moja ili babu yake auawe. Diwani wa Kata ya Mtowisa, Edger Malinyi naye amekaririwa … more »

Kiswahili chakwamisha kesi mahakakani

Charles Mullinda at M I K I T O – 4 days ago
ARUSHA Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) leo imeshindwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kwa sababu hati ya mashitaka imeandaliwa kwa Lugha ya Kiswahili. Baraza la Serikali ya Kijiji cha Ololosokwan kilicho Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha limefungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania likiiomba EACJ iizuie Serikali kuwahamisha kwenye ardhi wanayoishi. Shauri hilo liko mbele ya majaji watatu wa EACJ wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi ambaye aliahirisha shauri hilo kwa maelezo kuwa hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakama… more »

GODBLESS LEMA, MALISA WANAPOMZABUA BASHE

Charles Mullinda at M I K I T O – 1 week ago
*MACHI 6, 2018* *Haya ni maoni ya Malisa GJ na Godbless Lema kuhusu barua ya Hussein Bashe kwenda kwa Katibu wa Bunge akitaka iundwe kamati teule ya kibunge kuchunguza matukio yanayohatarisha usalama wa Watanzania. * Malisa Anaandika MALISA GJ November 2017 BASHE: Chadema wakiwachokoza wapigeni bila huruma. Wapigeni sana maana Jeshi la Polisi na vyombo vya dola vipo chini yetu. February 2018 Agizo likatekelezwa. Watu wakapigwa bila huruma. Raia wakapigwa risasi, wakauawa, wakajeruhiwa, wakatekwa, wakapotezwa. March2018 BASHE: Nimepeleka hoja bungeni ili kamati teule ya bunge ich… more »

HUSSEIN BASHE ANAPOTUHUMIWA UNAFIKI?

Charles Mullinda at M I K I T O – 1 week ago
MACHI 6, 2018 Bashe *Bashe Mohamed Bashe, ambaye ni Mbunge wa Nzega Mjini CCM, mara kadhaa amekuwa akiibua mijadala katika mitandao ya kijamii kwa kuandika akieleza misimamo na mitazamo yake kuhusu mambo mbalimbali yanayotokea hapa nchini.* *Watu wengi na hasa wana CCM wenzake wamekuwa wakiitafasili misimamo na mitizamo yake kuwa yenye sura au vimelea vya upinzani dhidi ya chama chake. * *MIKITO BLOG imeanza kufuatilia mijadala inayotokana na misimamo na mitizamo ya mwanasiasa huyo machachari wa CCM kwa lengo la kuibua mjadala mpana zaidi kuhusu aina ya siasa zinazofanywa na Bashe…. more »

MBOWE ATOKA HOSPITALINI

Charles Mullinda at M I K I T O – 1 week ago
MACHI 6, 2018 Mbowe MOSHI MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana usiku aliruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa akitibiwa na kurejea nyumbani. Mbowe alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, baada ya kujisikia vibaya ghafla ikiwa ni saa chache kabla ya kuripoti polisi, yeye na viongozi wenzake sita wa Chadema kama walivyotakiwa na polisi. Taarifa za kitabibu zilizopatikana jana, zilieleza kuwa alipofikishwa hospitali hapo alikuwa akilalamika kusumbuliwa na maumivu ya kichwa na baada ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika kuwa anasumbuliwa na… more »

MAHAKAMA YATUPA OMBI LA HOSPITALI YA KAIRUKI

Charles Mullinda at M I K I T O – 1 week ago
MACHI 6, 2018 DAR ES SALAAM Ombi lililowasilishwa na Hospitali ya Kairuki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa kesi ya madai inayoikabili isikilizwe kwa siri limetupiliwa mbali. Hospitali ya Kairuki iliiomba mahakama isikilize kesi hiyo dhidi yake bila waandishi wa habari kuruhusiwa kuiripoti. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba jana alitupilia mbali ombi hilo kwa kueleza kuwa vifungu vya sheria vilivyowasilishwa katika maombi hayo haviendani na shauri lililopo mahakamani. Hakimu Simba alisema sheria inaruhusu kesi zote za madai kuendeshwa … more »

MILIONI 18 ZAMLIZA MBUNGE WA CCM

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 5, 2018 Mbunge Tweve IRINGA Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Iringa, Rose Tweve, leo amelia machozi hadharani baada ya kupewa shuilingi milioni 18 kwa ajili ya mradi ya maendeleo ya akina mama. Tweve amepewa fedha hizo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Salimu Asas mbele ya wajumbe wa Bara za Wanawake (UWT) la CCM, Wilaya ya Mufindi ukiwa ni mchango wake kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya akina mama. Asas aliamua kutoa fedha hizo kumuunga mkono Tweve ambaye aliyetoa sh. 600,000 kwa kata 17 za wilaya hiyo kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananch… more »

Nusu kaputi = Nusu kuua

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 5, 2018 Dk. Mpoki DAR ES SALAAM Maneno nusu kaputi yanalotumiwa na watalaamu wa dawa za usingizi yanamaanisha kumuua mtu nusu na nusu nyingine anabaki akiwa hai. Tafasili ya maneno hiyo imetoleana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya tatu kwa wataalamu wa dawa za usingizi jijini Dar es Salaam leo. Dk Mpoki alisema neno hilo ni baya kwa sababu linawaogopessha wagonjwa wanaotakiwa kufanya upasuaji ambao ni lazima wapatiwe dawa hiyo ya usingizi. Aliwashauri watalaamu hao kuwa,… more »

111 AKIWAMO DIWANI WAPUKUTIKA CHADEMA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Gervas Mwakyusa muda mfupi baada ya kusajili wa CCM akitokea Chadema MACHI 4, 2018 Wanachama 110 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekihama chama hicho leo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sambamba nao, Garvas Mwakyusa, Diwani wa Kata ya Legezamwendo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa kwa tiketi ya Chadema naye amejivua wadhfa wake pamoja na uanachama na kujiunga na CCM. Taarifa kutoka mkoani Rukwa zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika mkutano wa ndani wa CCM wa ujenzi wa chama katika Wilaya ya Kalambo ulioongozwa na Katibu Mwenez… more »

ZITTO ZIARANI TABORA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 4, 2018 ZIARA YA KIONGOZI WA CHAMA CHA ACT – WAZALENDO KATIKA KATA YA USINGE, WILAYA YA KALIUA MKOANI TABORA

Untitled

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 4, 2018 MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI ILIYOANDALIWA NA TRA KUHUSU MASUALA YA KODI. SEMINA HIYO ILIFANYIKA JANA KATIKA UKUMBI WA BENKI KUU YA TANZANIA

‘WANASIASA MWACHENI AKWILINA APUMZIKE KWA AMANI’

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 3, 2018 DODOMA Wanasiasa wameonywa waache kuutumia kisiasa msiba wa mwanafunzi Akwilina Akwilini ili apumzike kwa amani. Akwilina aliuawa mwezi uliopita baada ya kupigwa risasi wakati polisi wakitawanya maandamano ya wanachama na mashabiki wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mbali na wanasiasa, wengine walioonywa kuacha kuutumia msiba huo kwa malengo yao ni makundi yote yanayotumia mwamvuli wa wanasiasa. Onyo hili limetolewa jana na Mwenyekiti Jumuiya ya Taasisi za Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) George Mnali katika mkutano wa tamati tendaji ya umoja huo… more »

SIMBA, FISI WALISHWA SUMU

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 3, 2013 kundi la Simba DODOMA Simba sita na Fisi zaidi ya 100 wamekufa baada ya kulishwa simu iliyowekwa kwenye nyama pembezoni mwa Hifadhi ya Ruaha. Pamoja na wanyama hao, ndege zaidi 100 nao wamekufa baada ya kula mizoga ya Simba na Fisi iliyowekewa sumu na wafugaji, wiki tatu zilizopita. Mauaji hayo ya wanyama wamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalaah alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani mjini hapa. Kundi la Fisi Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri Kigwangallah alieleza kusitikishwa na mauaji hayo ya w… more »

Diwani wa Zitto alivyosajiliwa CCM

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 3, 2018 MWENYEKITI WA Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Manyara, Saimon Lulu (aliyevaa suti ya rangi ya kijivu) akijiandaa kumkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Diwani wa Kata ya Gehandu katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Mathayo Samhenda baada ya kujivunia uanachama wa ACT-Wazalendo, jana. Mathayo Samhenda akionyesha kadi ya CCM aliyokabidhiwa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa, Saimon Lulu, jana. Mbunge wa Hanang, Mary Nagu wa kwanza kushoto na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Manyara Saimon Lulu wakimshangilia Mathayo Samhenda baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM,… more »

ZITTO AZIDI KUACHWA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 3, 2018 ZITTO AZIDI KUACHWA Zitto Kabwe DAR ES SALAAM Taarifa zilizotufikia kutoka Kata ya Gehandu, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara zinaeleza kuwa Diwani ya Chama cha ACT-Wazalendo wa kata hiyo, Mathayo Samhenda, amejiuzulu udiwani na kujivua uanachama wa chama chake muda mfupi uliopita. Zimeeleza kuwa diwani huyo baada ya kujiuzulu na kujivua uanachama wa ACT- Wazalendo ametangaza kujiunga na CCM. Taarifa kutoka Hanang zimeeleza kuwa kujiuzulu kwa diwani huyo kumekuja ikiwa ni siku chache baada ya kumkabili ana kwa ana Kiongozi wa chama, Zitto Kabwe na kumweleza kutoridhika n… more »

ORODHA YA WATZ WAUZA ‘UNGA’ WALIONYONGWA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 3, 2018 ORODHA YA WATZ WAUZA ‘UNGA’ WALIONYONGWA NA KUFUNGWA MAISHA DAR ES SALAAM Watanzania 14 waliokamatwa na madawa ya kulevya katika nchi mbalimbali duniani wamenyongwa hadi kufa. Sambamba na hao, Watanzania wengine 12 waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara hiyo wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia MIKITO BLOG kutoka Kitengo cha Dawa Kulevya Zanzibar, walionyongwa ni Juma Omar Mgeni ambaye hajatatwa makazi yake, Masumbuko Salum Hassan mkazi wa Dar es Salaam, Salum Mohammed Kitupura mkazi wa Dar es Salaam, John James Aman… more »

ZITTO AACHIWA ‘NYUMBA’

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 2, 2018 ZITTO AACHIWA ‘NYUMBA’ Zitto Kabwe DAR ES SALAAM Waasisi wawili wa Chama cha ACT- Wazelendo na viongozi waandamizi 10, leo wamekipa kisogo chama hicho wakikiacha mikononi mwa Kiongozi Mkuu, Zitto Kabwe wanayemtuhumu kutoa kauli za kuhamasisha Serikali iliyoko madarakani iangushwe. Tukio hilo lilitokea jana asubuhi katika Hotel ya Silver Paradise, iliyopo Tip Top, Masenze ambako walifanya mkutano na waandishi wa habari, walioundaa kwa ajili ya kutangaza uamuzi wao. Waliokipa kisogo ACT- Wazalendo ni Ramadhani Ramadhani, aliyekuwa Makamau Mwenyekiti wa Kwanza wa Taifa (… more »

NYONGO ATAKA MADINI YA NICKEL YAONGEZWE THAMANI

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 2, 2018 NYONGO ATAKA MADINI YA NICKEL YAONGEZWE THAMANI NCHINI Meneja Mkazi wa Mradi wa Kabanga Nickel, Andrew Msola akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa mradi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ambaye yuko katika ziara ya kikazi wilayani humo. NGARA Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema Serika itaboresha mazingira ya uwekezaji wa Madini ya Nickel yanayopatikana Ngara mkoani Kagera ili kuwawezesha wawekezaji kuyaogezea thamani kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi. Aliyasema hayo jana alipotembelea Mradi… more »

KAKONKO WAOMBA WATAALAM WA MIAMBA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 2, 2018 KAKONKO WAOMBA WATAALAM WA MIAMBA Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo KAKONKO Wananchi wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma wameiomba Serikali isaidie kuwapatia wataalam wa miamba watakaotafiti na kubainisha kiasi cha madini yaliyogundulika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Akiwasilisha taarifa ya wilaya kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ambaye yuko katika ziara ya kikazi wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala alisema Madini ya Dhahabu yamegundulika katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Alitaj… more »

NDEGE ZA SERIKALI ZATENGEWA BILIONI 11

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
MACHI 2, 2018 NDEGE ZA SERIKALI ZATENGEWA BILIONI 11 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiteremka baada ya kukagua mojawapo ya ndege za Wakala wa Ndege za Serikali alipotembelea wakala hiyo leo. DAR ES SALAAM Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) imetengewa Shilingi Bilioni 11.4 kwa ajili ya kuboresha huduma zake. Akizungumza na Menejimenti ya TGFA jana, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa majukumu ya wakala hiyo, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye al…more »

MADIWANI WA CHADEMA WAFICHWA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Machi 2, 2018 MADIWANI WA CHADEMA WAFICHWA Joseph China MBEYA Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wakitajwa kuwa na nia ya kukihama chama hicho kwenda kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) walichukuliwa na kufichwa eneo la siri ili wasitekeleze azma yao. Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Joseph China ndiye aliyethibitisha kufichwa kwa madiwani hao wakati akizungumza na waandishi wa habari wiki hii. China aliwaeleza waandishi wa habari kuwa baada ya kusikia tetesi kuhusu mpango wa madiwani hao kuhamia CCM aliitisha kikao cha dharura cha madiwani w… more »

Mbowe na Zitto yameisha

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Mbowe na Zitto yameisha Zitto akiwa na Mbowe DAR ES SALAAM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amekubali kumpokea na kumrejeshea unachama wa chama hicho, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe. Imeekezwa. Mbowe amekubali kumpokea Zitto baada ya kufanya mazungumzo wakiwa nje ya nchi na kumpa masharti ya kurejea ambayo Zitto aliyakubali. Mbowe aliingia kwenye mgogoro na Zitto pale alipotangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema uliosababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama kabla wazee kuingilia kati kisha Zitto akatimuliwa. Mmoja wa … more »

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI, STANSLAUS NYONGO, KAGERA

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI, STANSLAUS NYONGO KATIKA MGODI WA HAMAD MINE SCALE ULIOPO WILAYA YA KWERWA, MKOA WA KAGERA Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mwenye Kaunda Suti- mbele) na Ujumbe wake, baada ya kukagua mitambo inayotumika kusaga mawe yenye Madini ya Bati (kulia) katika Mgodi wa Hamad Mine Scale, uliopo eneo la Omukasheni, Wilaya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera, Februari 28 mwaka huu, akiwa katika ziara ya kazi. Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), akikagua madini ghafi ya Bati (aliyoshika mkononi) na kuzungumza na mmoja… more »

Dk. Kijo-Bisimba atakiwa kupima kauli zake

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Dk. Kijo-Bisimba atakiwa kupima kauli zake DAR ES SALAAM UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umemtaka Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba kupima kauli zake za kuishutumu Serikali kwa sababu haziendani na umri wake. Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka ndiye aliyetoa kauli hiyo jana alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC. Katika mahojiano hayo, Shaka alisema huenda Dk. Bisimba amefurahishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka damu imwagike au yatokee… more »

Rufaa ya ‘Sugu’ yakamilika

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Rufaa ya ‘Sugu’ yakamilika MBEYA MAWAKILI wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) na Katibu Kanda ya Nyasa Emmanueli Masonga, wamekamilisha taratibu za ukataji wa rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya. Mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula jana alieleza kuwa tayari wameshakamilisha taratibu zote muhimu za kukata rufaa hiyo wanachosubiri ni kupangiwa tarehe na Mahakama Kuu. Wakili Mangula alieleza kuwa ni anatumaini mahakama itapanga haraka tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya Sugu. Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa E… more »

Waziri Mkuu Majaliwa ataka udhibiti mimba

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Waziri Mkuu Majaliwa ataka udhibiti mimba za utotoni TANDAHIMBA WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa kuwepo kwa udhibiti wa mimba za utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba. Akizungumza jana na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, alisema ni lazima viongozi wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike wa wilaya hiyo dhidi ya mimba ili waendelee na masomo. “Kwa nini kila mwaka mimba Tandahimba zinaongezeka, viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi. “Lazima wahusika wote wakamatwe wachukuliwe hatua kwa m… more »

Mtaka alaumu mashirika ya afya

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Mtaka alaumu mashirika ya afya SIMIYU MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka ameyalaumu mashirika ya afya yaliyopo Mkoa wa Simuyu kwa kushindwa kutatua changamoto za afya kwa wananchi. Lawama hizo alizitoa katika kikao cha wadau wa afya mkoani Simiyu kilichoshirikisha mashirika yote. Alisema wingi wa mashirika hayo ni kiashiria cha kuwepo matatizo mengi ya afya mkoani Simiyu.

Vipodozi vikali chanzo cha saratani

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Vipodozi vikali chanzo cha saratani DAR ES SALAAM Matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu yanasababisha ugonjwa wa saratani. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grace, Elizabeth Kilili alipokuwa akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam. Alisema vipodozi vyenye sumu vinasababisha saratani ya ngozi, kuua nguvu za kiume na kuharibu ukuaji wa mtoto aliye tumboni.

Waziri Mkuu aagiza mapambano

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Waziri Mkuu aagiza mapambano dhidi ya uhalifu soko la korosho MTWARA Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho. Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba. Alisema Wilaya ya Tandahimba ina korosho za daraja la kwanza hivyo ni ajabu kuona korosho chafu na kuhoji zinatokea wapi. Awali, Waziri Mkuu Majaliwa alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms alikotoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho kufunga mashine … more »

Kubenea hana imani na polisi

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Kubenea hana imani na polisi DAR ES SALAAM Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea jana alidai kuwa haliamini Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa matukio yanayokihusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kubenea alitoa madai hayo jana Dar es Salaam kwa kueleza kuwa polisi wamekosa sifa na hawaaminiki tena. Alidai kusikitishwa na polisi kwa sababu wanavunja sheria za nchi.

Watatu Chadema kortini

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Watatu Chadema kortini DAR ES SALAAM Watu watatu waliokuwa wakishikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jana walifikishwa kortini wakituhumiwa kufanya mkusanyiko usiokuwa halali. Watuhumiwa hao ambao wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa. Walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, aliyeieleza mahakama wanaunganishwa na wenzao 28 walioshtakiwa wiki iliyopita. Wakili Mwita alidai mahakamani kuwa washtakiwa walifanya mkusanyiko…more »

Serikali, washirika wa maendeleo

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Serikali, washirika wa maendeleo kurejesha uhusiano *Na Benny Mwaipaja, Dodoma* *Serikali imekubaliana na washirika wa maendeleo kurejesha uhusiano wa karibu na wenye tija ili kusaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano na Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanzibar (MKUZA III).* *Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa mazungumzo ya kimkakati baina ya Serikali na washirika wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali duniani, mjini Dodoma mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James alisema mwongozo wa ushirikiano wa ma… more »

Wiki ya mlipa kodi kuanza Machi 5

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Wiki ya mlipa kodi kuanza Machi 5 Wiki ya elimu kwa mlipa kodi inatarajiwa kuanza Machi 5 hadi 9 katika mikoa yote nchini. Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Koyombo, lengo lililokusudiwa ni katika wiki hiyo ni kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto na kupokea mrejesho na maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi. Alisema pamoja na masuala mengine, TRA itatumia wiki hiyo kutoa elimu ya ulipaji kodi ya majengo kwa njia ya kielektroniki, elimu kuhusu mkataba wa huduma kwa mlipa kodi na matumizi sahihi na umuhimu w… more »

madiwani wawili Chadema wakimbia

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Madiwani wawili Chadema Serengeti wakimbilia CCM Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, jana walitangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Madiwani hao, Joseph Mongita wa Kata ya Manchira na Michael Kunani wa Kata ya Ikoma walitangaza uamuzi huo jana mjini hapa. Katika tamko lao la kukihama Chadema, walisema mbali ya kujiuzulu udiwani, pia wamejivua nyadhifa zao zote ndani ya Chadema. Walisema, wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa Chadema siyo tena chama cha siasa kama ilivyokuwa awali na kwamba hivi sasa hak… more »

Untitled

Charles Mullinda at M I K I T O – 2 weeks ago
Mwanamuziki Misri afungwa kwa kukashifu Mto Nile Mwanamuziki maarufu wa Misri, Sherine Abdel Wahab amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kukashifu usafi wa Mto Nile. Sherine ambaye pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji yanayojulikana kwa jina la The Voice alitiwa hatiani na mahakama wiki hii baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuukashifu Mto Nile. Ilidaiwa mahakamani kuwa mwanamuziki huyo, aliwaambia wapenzi wa mashabiki wake wakati wa onyesho lake nchini huko kwamba kunywa maji ya Mto Nile kunaweza kumpatia vijidudu. Sherine alifunguliwa mashitaka mwezi Novem… more »
Previous article
Next article

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya