Wednesday, December 25, 2024
spot_img

MBOWE ATOKA HOSPITALINI

MACHI 6, 2018
Mbowe

MOSHI 
MWENYEKITI  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, jana usiku aliruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa akitibiwa na kurejea nyumbani.
Mbowe alilazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, baada ya kujisikia vibaya ghafla ikiwa ni saa chache kabla ya kuripoti polisi, yeye na viongozi wenzake sita wa Chadema kama walivyotakiwa na polisi.
Taarifa za kitabibu zilizopatikana jana, zilieleza kuwa alipofikishwa hospitali hapo alikuwa akilalamika kusumbuliwa na maumivu ya kichwa na baada ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika kuwa anasumbuliwa na uchovu.
Akiwa hospitalini hapo aliwekewa mashine ya oksijeni kwa ajili ya kumsadia kupumua.
Afisa Uhusiano wa KCMC , Gabriel Chisseo amekaririwa akieleza kuwa Mbowe aliruhusiwa na madaktari kutoka hospitali muda wa 1:30 usiku baada ya kujiridhisha kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema naye alizungumzia kuimarika kwa afya ya Mbowe lakini alisema hajui alipo.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya