MACHI 5, 2018
Mbunge Tweve |
IRINGA
Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Iringa, Rose Tweve, leo amelia machozi hadharani baada ya kupewa shuilingi milioni 18 kwa ajili ya mradi ya maendeleo ya akina mama.
Tweve amepewa fedha hizo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Salimu Asas mbele ya wajumbe wa Bara za Wanawake (UWT) la CCM, Wilaya ya Mufindi ukiwa ni mchango wake kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya akina mama.
Asas aliamua kutoa fedha hizo kumuunga mkono Tweve ambaye aliyetoa sh. 600,000 kwa kata 17 za wilaya hiyo kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananchi.
Imeelezwa kuwa lengo Tweve ni kutoa Sh. Milioni 60 kwa kata zote za Mkoa wa Iringa.
Assas baada ya kutoa kiasi hicho cha fedha alisema amefurahishwa na mkakati wa Tweve wa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini wanaostahili kuinuliwa kiuchumi.
Tweve baada ya kupokea fedha hizo huku machozi yakimbubujika alisema anajisikia furaha na amani kuona watu wanathamini mchango wake katika jamii na kumuunga mkono.