Gervas Mwakyusa muda mfupi baada ya kusajili wa CCM akitokea Chadema |
MACHI 4, 2018
Wanachama 110 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekihama chama hicho leo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Sambamba nao, Garvas Mwakyusa, Diwani wa Kata ya Legezamwendo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa kwa tiketi ya Chadema naye amejivua wadhfa wake pamoja na uanachama na kujiunga na CCM.
Taarifa kutoka mkoani Rukwa zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika mkutano wa ndani wa CCM wa ujenzi wa chama katika Wilaya ya Kalambo ulioongozwa na Katibu Mwenezi wa CCM, Taifa Humphrey Polepole.
Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza katika mkutano wa ndani kwenye Kata ya Lugezamwendo wilayani Kalambo, leo. |
Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo |