Wednesday, December 25, 2024
spot_img

NYONGO ATAKA MADINI YA NICKEL YAONGEZWE THAMANI


MACHI 2, 2018
NYONGO ATAKA MADINI YA NICKEL YAONGEZWE THAMANI NCHINI

Meneja   Mkazi   wa   Mradi   wa   Kabanga   Nickel,   Andrew   Msola akiwasilisha   taarifa  ya utendaji kazi wa mradi  huo   kwa   Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ambaye yuko katika ziara ya kikazi wilayani humo.


NGARA
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema Serika itaboresha   mazingira   ya   uwekezaji   wa   Madini   ya   Nickel yanayopatikana   Ngara   mkoani   Kagera ili kuwawezesha wawekezaji kuyaogezea thamani kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.
Aliyasema hayo jana alipotembelea Mradi wa Uwekezaji wa Madini ya Nickel wa Kabanga, uliopo Wilaya ya Ngara, Mkoa wa Kagera.
“Sisi Serikali tutahakikisha tunawaletea wawekezaji miundombinu ya   barabara, reli na umeme ili kuwajengea mazingira rafiki ya uzalishaji lakini   kwa upande wao  tunataka kuona uwekezaji makini.
“Wachimbe na kuongeza thamani ya madini hayo hapa nchini. Badala ya kutoa Nickel kama malighafi, watoe bidhaa zinazotokana na Nickel,” alisema Nyongo.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha madini hayo muhimu ambayo kwa sasa soko lake duniani limeanza kupanda, yanalinufaisha taifa kwa kiwango kinachostahili.
“Tunataka wawekezaji wachimbe ili tupate kodi, tupate mrabaha lakini pia wananchi wa maeneo haya waweze kupata ajira,” alisema.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Mradi wa Kabanga Nickel,   Meneja   Mkazi, Andrew Msola alisema changamoto waliyonayo ni ukosefu wa miundombinu barabara, reli na umeme.
Mradi   wa   Kabanga Nickel ulianza uzalishaji wa Madini ya Nickel zaidi ya miaka 40 iliyopita lakini tangu mwaka2009 ilisimamisha uzalishaji kutokana na kuporomoka kwa bei ya madini hayo katika Soko la Dunia.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael Mlengele, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Mbunge wa Ngara,   Alex   Gashaza   na   Afisa   Madini   Mkazi   wa   Mkoa wa Kagera,   Daniel Mapunda,   wakiwa   katika   kikao   na  wawekezaji   wa   Mradi   wa Kabanga   Nickel, jana.

Sehemu ya shehena ya Madini ya Nickel.



Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya