Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule.
“Watakaobainika kuwafungia ndani watoto wenye mahitaji maalumu wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanawakosesha haki ya kupata elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa ataka udhibiti mimba
Waziri Mkuu Majaliwa ataka udhibiti mimba za utotoni
TANDAHIMBA
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa kuwepo kwa udhibiti wa mimba za utotoni katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Akizungumza jana na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, alisema ni lazima viongozi wasimamie nidhamu kwa kuwalinda watoto wa kike wa wilaya hiyo dhidi ya mimba ili waendelee na masomo.
“Kwa nini kila mwaka mimba Tandahimba zinaongezeka, viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.
“Lazima wahusika wote wakamatwe wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria kwa sababu wanaharibu elimu ya mtoto wa kike,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.