Tuesday, December 24, 2024
spot_img

Rufaa ya ‘Sugu’ yakamilika

Rufaa ya ‘Sugu’ yakamilika

MBEYA

MAWAKILI wa Mbunge wa Mbeya Mjini,  Joseph Mbilinyi (Chadema) na Katibu Kanda ya Nyasa Emmanueli Masonga, wamekamilisha taratibu za ukataji wa rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya.
Mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula jana alieleza kuwa tayari wameshakamilisha taratibu zote muhimu za kukata rufaa hiyo wanachosubiri ni kupangiwa tarehe na Mahakama Kuu.
Wakili Mangula alieleza kuwa ni anatumaini mahakama itapanga haraka tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya Sugu.


Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, walihukumiwa kifungo cha miezi mitano  gerezani bila faini baada ya kukutwa na hatia ya kutamka maneno ya fedheha yaliyomlenga Rais Dk. John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30, mwaka 2017 katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Mwenge ya jijini Mbeya.

 

 

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya