Tuesday, December 24, 2024
spot_img

Mbowe na Zitto yameisha

Mbowe na Zitto yameisha
 

Zitto akiwa na Mbowe

DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amekubali kumpokea na kumrejeshea unachama wa chama hicho, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe. Imeekezwa.
Mbowe amekubali kumpokea Zitto baada ya kufanya mazungumzo wakiwa nje ya nchi na kumpa masharti ya kurejea ambayo Zitto aliyakubali.
Mbowe aliingia kwenye mgogoro na Zitto pale alipotangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema uliosababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama kabla wazee kuingilia kati kisha Zitto akatimuliwa.
Mmoja wa watu wa karibu na Zitto ambaye pia alikuwa mshirika wake katika harakati za siasa za upinzani kabla ya kuhasimiana, ameeleza kuwa Mbowe na Zitto walikutana jijini Nairobi nchini Kenya ambako walifanya mazungumzo ya kina kabla ya kufikia makubaliano.
Msiri huyo ambaye anamtaja Zitto kuwa mwanasiasa machachari asiyetabirika, asiyeaminika na asiyepaswa kutegemewa, ameamua kujiunga na siasa za kianaharakati kama zile zinazofanywa na Chadema baada kutotimia kwa matarajio aliyokuwa nayo ya kuwa mmoja wa wanasiasa wa upinzani kuteuliwa kuwa viongozi waandamizi wa Serikali.
Katika andiko lake ambalo limevuja na kusambazwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii, msiri huyo wa Zitto ameandika kuwa wawili hao walikutana Nairobi wakiwa na viongozi wengine wa Chadema anaowataja kuwa ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.
Mmwenyekiti wa Chadema  Freeman Mbowe, Mbunge na Tarime Vijijini, John Heche wakiwa  na Kiongozi Mkuu wa Act-Wazalendo  Zitto Kabwe,  Nairobi Kenya 

“Najua kwamba hitaji lake yeye, ilikuwa ninyi mkukubali aingize ACT kwenye UKAWA lakini Mbowe ukakataa kwa sababu zinazojulikana ambazo hazitofautiani na zilizomfanya akamkatalie Lowassa kuileta ACT katika ushirika wa UKAWA mwaka 2015.
“Ulijenga hoja kwamba ACT inakufa kwa kuondoka akina Kitila Mkumbo hivyo ni bora yeye Zitto arejee Chadema peke yake na iwapo ana wafuasi wake, watamfuata!
“Hakuwa na jinsi, ilibidi akubaliane na hilo. Najua mlikubaliana kimsingi kwenye hilo ila bado mkajipa muda wa kuonana tena na kukamilisha mazungumzo ikiwa ni pamoja na ratiba ya utekelezaji wa hilo,” linasomeka andiko hilo la msiri wa Zitto.
Anaandika zaidi kuwa Mbowe anafurahia kurejea kwa Zitto kwa sababu amemzidi katika siasa za kiuanaharakati.
Kwamba hivi sasa Zitto amekuwa akitoa maneno makali dhidi ya Serikali ambayo anaogopa kuyasema dhidi ya Serikali na Rais wa nchi.
“Nilicheka sana kumwona kwenye mitandao akiwahamasisha wabunge na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wasaini ‘petition’ ambayo sijui alikuwa anaiandaa yeye ili kukulazimisha wewe na viongozi wenzako wa juu wa Chadema muitishe kikao cha Kamati Kuu na kufanya uamuzi mzito (ambayo pia angewaambia yeye uamuzi gani mfanye) na akaahidi eti yeye na chama chake kitawaunga mkono!
“Hii haijapata kutokea. Kiongozi wa juu kabisa wa chama A anahamasisha viongozi wa chama B waasi dhidi ya uongozi wao na kulazimisha kikao ili wafanye kikao na kufanya maamuzi yanayopendekezwa na kiongozi huyo kwa ahadi kwamba atawaunga mkono!!!
“Si aitishe kamati kuu yake afanye hayo maamuzi magumu halafu aombe chama chenu kimuunge mkono!!? Ajabu hata kukusindikiza tu polisi hajaenda,” inasomeza sehemu ya andishi la msiri wa Zitto.
Katika hali isiyotarajiwa, msiri huyo wa Zitto anamshutumu kuwa mbinafsi na fisadi mambo yaliyomfanya atofautiane na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
David Kafulila
“Utakuwa unajua kwamba katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015, alikutana na watuhumiwa ufisadi wa Escrow kujadili njia za kumdhibiti Kafulila asirudi bungeni kwa sababu aliapa kufa na watuhumiwa hao.
“Lakini baada ya kuhakikisha Kafulila ameshindwa uchaguzi Kigoma Kusini na yeye akarudi bungeni kwa msaada wa rafiki zake wa ndani ya CCM, akaanza kuwasha moto tena akitaka mafisadi wa Escrow wakamatwe!
“Yote anapiga mkwara ili wamwite wampe kitu anyamaze,” anaandika zaidi.
Aidha, anaandika kufichua jinsi Zitto alivyotoa taarifa zisizo sahihi kwa Msajili wa Vyama vya  Siasa kuhusu fedha zilizotumiwa na ACT Wazalendo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“Zitto alisema kwa msajili wa vyama kuwa chama chake kilitumia jumla ya shilingi milioni 600 na kidogo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
“Sasa nenda kwa aliyekuwa Mweka hazina wa ACT Taifa akupe ripoti kamili ya fedha. Chama kilitumia milioni 72 kwenye kampeni za urais nilizosimamia mimi.
Zitto akiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za 2015
“Lakini kwenye kampeni za ubunge alizosimamia yeye, chama kilitumia bilioni 1, milioni 144,” anazidi kuandika.
Sehemu nyingine ya andiko lake inayohusu chuki ya Zitto dhidi ya Serikali inasomeka hivi; “Leo anakuambia anamchukia Rais Magufuli. Si yeye aliyebaki bungeni wakati nyinyi mnatoka na kususia hotuba ya rais ya kuzindua Bunge?
“Si yeye aliyemsifia Rais kwa hotuba yake na kusema imesheheni ilani ya ACT kwa asilimia 60? Si yeye aliyemsifia wakati akimtumbua Prof. Muhongo (Sospeter) kwenye ripoti za Makinikia?
“Si yeye aliyewananga mlipopinga sheria za madini kwa hati ya dharura?… anamchukia Rais Magufuli kimkakati. Mfano: Alipobaki bungeni na kuhudhuria kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Dodoma, alikuwa amepigwa changa la macho na marafiki zake wa ndani ya CCM kwa Magufuli (Rais) angewateua watu wake fulani toka ACT kuwa wabunge mwanzoni kabisa mwa utawala wake.
“Lakini alipomchukia Magufuli (Rais) mwanzoni kabisa na kuanzisha Operesheni Linda Demokrasia ni baada ya uteuzi wa wabunge kukwama kisha akaenda kuangalia kwenye orodha ya kamati za bunge akakuta amepangwa kwenye kamati ya huduma za jamii na siyo hesabu za serikali na rafiki yake mmoja akamwambia eti ni maelekezo ya Rais.
“Lakini pia marafiki zake waliokuwa wanaongoza mashirika ya umma na kumpa hela wakatumbuliwa.
“Alipomsifia sana Rais Magufuli, wakati wa kupelekwa sheria za madini kwa hati ya dharura na hatimaye akamsifia sana kule Kigoma alikofanya ziara Rais, ni kwa sababu alikuwa ameahidiwa na wapambe wake kwamba Rais akirudi tu Dar, anamteua kumrithi Muhongo uwaziri wa Nishati na Madini.”

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya