Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara, jana walitangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Madiwani hao, Joseph Mongita wa Kata ya Manchira na Michael Kunani wa Kata ya Ikoma walitangaza uamuzi huo jana mjini hapa.
Katika tamko lao la kukihama Chadema, walisema mbali ya kujiuzulu udiwani, pia wamejivua nyadhifa zao zote ndani ya Chadema.
Walisema, wamefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa Chadema siyo tena chama cha siasa kama ilivyokuwa awali na kwamba hivi sasa hakijulikani kama ni chama cha siasa au kikundi chenye malengo tofauti ya kufanya lolote ilimradi kifike Ikulu.
Kwamba Chadema ya sasa ni kikundi kinachopinga kila kitu hata yake ambayo kiliwahi kuyaahidi kuyasimamia lakini kwa sababu sasa yanafanywa na Serikali ya CCM kinayapinga.
madiwani wawili Chadema wakimbia
Madiwani wawili Chadema Serengeti wakimbilia CCM