Tuesday, December 24, 2024
spot_img

Mwanamuziki Misri afungwa kwa kukashifu Mto Nile


Mwanamuziki maarufu wa Misri, Sherine Abdel Wahab amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kukashifu usafi wa Mto Nile.
Sherine ambaye pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji yanayojulikana kwa jina la The Voice alitiwa hatiani na mahakama wiki hii baada ya kushitakiwa kwa kosa la kuukashifu Mto Nile.
Ilidaiwa mahakamani kuwa mwanamuziki huyo, aliwaambia wapenzi wa mashabiki wake wakati wa onyesho lake nchini huko kwamba kunywa maji ya Mto Nile kunaweza kumpatia vijidudu.
Sherine alifunguliwa mashitaka mwezi Novemba mwaka jana baada ya video yake kusambazwa mtandaoni ikimuonyesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya Mto Nile?).
Katika video hiyo, Sherine alionekana akiwajibu wapenzi na mashabiki wake kuwa ‘Nikinywa maji ya Mto Nile nitapata kichocho.’
Nchini Misri, ugonjwa wa kichocho unawapata zaidi wananchi wa vijijini.
Aidha, chama cha wanamuziki nchini Misri kimetangaza kuupiga marufuku marufuku wimbo huo kuibwa Misri.
Wakati huo huo, mwanamuziki mwingine, Laila Amer naye mapema wiki hii alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya uchochezi, ufitini na uovu.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya