![]() |
Dk. Mduma |
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amemteua Dk. John Mduma kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda kwa vyombo vya habari leo, uteuzi wa Dk. Mduma unaanza kesho. Agosti 28, 2017.
Dk. Mduma ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Uchumi Vhuo Kikuu cha Dar es Salaam atakaimu nafasi baada ya Dk. Frederick Rindo kumaliza muda wake.