Ā
 |
Mkutano wa kampeni za CCM Igunga |
MWEZI mmoja wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga uliomalizika Oktoba Mosi umetuacha na fundisho kubwa la jinsi wanasiasa wetu hususan wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walivyo wa hovyo na wanavyopenda ukubwa kuliko kulitumikia taifa.
Katika kipindi hicho tumeshuhudia jinsi wanasiasa wa CCM walivyo na pesa za kuhonga na kufanya kila aina ya anasa. Na kikubwa jinsi wanavyotumia vibaya madaraka tuliyowapa.
Ā
Tumeona kwa macho jinsi walivyo mabingwa wa kuhonga na hata walivyo wazinzi wa kupitiliza kiasi cha kufanya ngono na wake wa wanasiasa wenzao.
Ā
CCM, ambacho ninakichukulia kama mwalimu aliyekuwa akifundisha darasa linaloitwa Igunga Ā imekuwa mwalimu mzuri, imetufundisha namna wakubwa walivyo na mabavu ya kukiuka sheria za nchi pasipo vyombo vya dola kuwanyooshea kidole
Ā
Kupitia CCM nimeelimika kuwa ukiwa mwanaCCM mwenye kawadhfa fulani, ukisumbuliwa na polisi unaweza kuwatusi hata matusi ya nguoni kwa kukuzuia kufanya jambo lolote la kipuuzi.
Ukawakoromea kwa sauti kuu kuwa wanaweza kupoteza kazi kwa kusimamia sheria na kulinda usalama wa raia. Kuwa mwana CCM kumbe ni raha sana.
Waliokuwa na shaka na uwezo wa wanasiasa wazee katika kutekeleza majukumu yao, naamini kuwa sasa shaka yao imetoweka kwa sababu tumewashuhudia wanasiasa wazee ambao wana historia ya kulala bungeni jinsi walivyo machachari wanaposaka nafasi za wenzao kujumuika nao huko kwenye viti vya kunesanesa, vyenye kubembeleza wazee wa aina yao kulala usingizi wa mchana ambao hulipiwa posho ya kulala kazini na serikali.
 |
Wassira |
Binafasi nimejua kuwa kumbe babu Stephen Wassira sio mchovu, bado yuko ngangari. Ana uwezo mkubwa wa kusimama majukwaani na kuhubiri yale yale tuliyoyachoka huku akiwashambulia kwa maneno makali lakini yasiyokuwa wanasiasa wenye mvuto kwa jamii ili jamii inayowakubali iwakatae.
Kumbe ile kulala bungeni huwa ni kwa sababu ya kukosa kazi muhimu za kufanya. Ile mijadala inayoendelea bungeni huwa si muhimu sana na huwa āinamboaā kiasi cha kumletea usingizi na kwa sababu inaruhusiwa kulala bungeni, huwa analala fofofo hadi anafotolewa foto na vitoto vitukutu.
Ā Siamini tena kuwa kulala kwake bungeni, yeye na wazee wenzake walioshiba sana kunatokana na uchovu wa kilevi ambacho huwa wanatumia kila linapoingia giza wakiwa Dodoma. Nadhani pamoja na sababu niliyoitaja hapo juu pia ni staili ya kuhudhuria vikao vya Bunge.
Huwa wanafikisha ujumbe kwa wapiga kura wao kuwa walitafuta kura kwa shida baada ya kufika bungeni wanastahili kupumzika kwa kulala usingizi wa rasharasha ambao mlalaji hushtuka kila baada ya dakika kadhaa kabla ya kulala tena.
Ni darasani Igunga ambako tumejifunza jinsi wanasiasa wa CCM walivyo ndumila kuwili. Tumemuona jinsi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Aziz, ambaye alijivua ubunge kwa madai ya kuchoshwa kamasio kuchukizwa na siasa za kipuuzi za chama chetu alivyorejea jukwaani kukiunga mkono chama alichokisuta kwa kuendekeza mambo ya kipuuzi.
CCM ni mwalimu kiboko, kina mbinu maridadi sana za ufundishaji. Kwa sababu kinajua kuwa watu hawajaelewa vema somo la usanii wa kisiasa, basi kikaamua kuwafundisha kwa vitendo.
Kikamchukua Gamba Rostam, yule yule aliyekitusi kisanii akaenda kukipigia debe kisanii Igunga. Huo ndiyo usanii wa kweli katika siasa za CCM.
 |
Rostam akihutubia kampeni za CCM |
Na kutoka darasani Igunga, tumejifunza jinsi wakubwa ndani ya CCM walivyogawanyika katika makundi hasimu kiasi cha kundi moja kushindwa kutia mguu kwenye kampeni za chama licha ya kuwa na umuhimu kulingana na mwenendo wa sasa wa kisiasa hapa nchini.
Viherehere wote ndani ya chama ambao kwa kiherehere chao huwa wanawafurahisha sana Watanzania walipigwa marufuku kufika Igunga isijetokea kwa kiherehere chao wakaeleza yale yasiyotakiwa. Huko Igunga palikuwa kwa mafisadi na wenye magamba tu ndani ya CCM.
Kwa wanafunzi wazuri wa somo la siasa za kipuuzi, watakubaliana na mimi kuwa kampeni za takribani siku 30 huko Igunga, zimetufudisha jinsi serikali ya CCM ilivyo na pesa za kuchezea. Inazichezea kwa sababu haina mahali pa kuzipeleka. Imeziweka maalumu kwa ajili ya kuzichezea katika nyakati kamahizi za kusaka ukubwa.
Nikiwa mmoja wa wanafunzi hao ambaye ninapenda somo la siasa za kipuuzi na ambaye huwa ninajifunza kwa bidii, darasani Igunga nimejifunza kuwa serikali ina uwezo wa kumgawia kila mwananchi nguo, chumvi, mchele, sabuni, vitambaa vinavyofanana rangi na nguo za CCM, pesa tasilimu, kununulia wananchi pombe na hata kuwapikia wala, nyama na maharage ikiamua.
Kauli kwamba serikali ya CCM haina fedha ni uongo, ukweli ni kwamba ina pesa nyingi mno, ndiyo maana wakubwa kila leo wanazurura hapa na pale ulimwenguni kusalimia wakubwa wenzao na kubadilishana mawazo ya namna ya kuzitumia fedha nyingi walizonazo.
Ikiamua kila kijiji kinaweza kuwa na gari jipya kabisa la kubebea wagonjwa na wala sio Bajaj. Kwa wasioamini hili waingie darasani wafanye hesabu za kukokotoa shilingi bilioni tatu zilizotupwa Igunga katika muda wa mwezi mmoja zinaweza kununua Bajaj ngapi za kubeba wajawazito katika barabara mbovu kupitiliza.
Halafu wafanye tena hesabu wakokotoe bilioni tatu zinaweza kununua magari mangapi aina ya Toyota Land Cruiser, Mkonga ya kubeba wajawazito. Wakipata jumla, wazidishe mara miezi kumi na mbili na hapo ni bila kuweka gharama ya ukodishaji Helikopta.
Kwa bidii kubwa ya kujifunza kutoka CCM,Ā kimenielisha kuwa kutumia bastora kutaka kuua kwa kusaka ukubwa katika kipindi cha kampeni inaruhusiwa na hata kupanda kwenye majukwa ya kisiasa kuhubiri uongo ukiwa na ruksa.
Nilipoandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari āTunalelewa na CCM tunayaishi matendo yakeā katika safu hii ya mchokonozi wiki chache zilizopita nililenga kuwajuza Watanzania jinsi mafundisho ya hovyo ya chama chetu cha maulaji yalivyotuingia na tunavyofanya vizuri katika kuyatekeleza.
Waliokwazwa na uchokonozi ule na hata kutuma ujumbe mkali kwangu leo ni mashahidi wa nilichokieleza kwa matokeo ya uchaguzi ule. CCM ilikuwa lazima ishinde kutokana ujuha wa wana Igunga wengi, hususan wazee.
Ninasikitika kueleza hivyo lakini huo ndiyo ukweli ninaouamini ambao kwangu ni dhambi inayostahili adhabu ya mauti kuuficha.
Neno Juha kwa mujibu wa tafasili iliyo kwenye kamusi ya Kiswahili sanifu ni āupungufu wa uwezo wa kufikiri na kuelewa mambo.ā Kwangu mimi Igunga wapo watu ambao ni majuha ambao kutokana na upungufu wa uwezo wao wa kufikiri na kuelewa mambo, hawakuelewa kuwa mkusanyiko wa wanasiasa wa CCM katika jimbo lao kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu haukuwa wa kufanya kampeni, bali kuwafundisha kwa vitendo namna nzuri ya kuzini na wake za watu kwa kutumia ukubwa wa chama, kutoa na kupokea rushwa mbele ya Polisi wa TAKUKURU, kutumia madaraka vibaya na kila aina ya uchafu.
Hili la uzinzi nimekuwa nikilisema kila mara kwa sababu ni moja ya mambo ya hovyo ambayo wakubwa wa CCM wanayapenda hivyo huwa wanayafanya kwa staili ya ukiwa nacho kitumie ambayo imekuwa ikiigwa na lundo la wananchama na hivyo kukitia doa jeusi la uzinzi chama chetuĀ cha maulaji.
Nitashangaa mno siku nikimsikia rafiki yangu Rais Jakaya Kikwete au kiongozi yoyote wa CCM na serikali yake wakikemea vijana kuachana na tabia ya uzinzi kabla hawajamkea kwa kumfukuza kundini kiongozi mwenzao mzinzi aliyefumaniwa akizini huko Igunga ambaye kwa sasa anastahili tunzo ya ufundishaji bora somo la uzinzi msimu wa kampeni za uchaguzi.
Like this:
Like Loading...